KATIBU MKUU BAVICHA ATAKIWA KUFIKA POLISI SIMU KUTOKA KWA IGP MSAIDIZI

Habari  Viongozi!
Nimepigiwa simu na msaidizi wa IGP kuwa niende ofisini kukutana na kamanda wa Operesheni ili kujadili barua tuliyowaandikia.
Nimemwambia siwezi kwenda kwa sababu barua yetu inajieleza vya kutosha, na inahitaji majibu yao ili sisi tuendelee na shughuli zetu.
Pia nimemwambia inashangaza kwamba, wameshindwa kujibu barua lakini wametuma polisi kuja Makao Makuu ya BAVICHA na kwa hiyo siwezi kwenda ofisini kwake, ila nakwenda ofisini nikaonane na hao waliowatuma ofisini kwangu.
Hadi sasa nipo ofisini na Mwenyekiti Mhe. Patrobas Katambi, na kuna mapolisi wamezingira ofisini kwetu hapa.
Tutawaeleza nini kitafuata kuanzia sasa.
Julius Mwita
Katibu Mkuu Bavicha


Maoni