WANANCHI WA TANZANIA WAMLALAMIKIA DKT MAGUFULI KUHUSU DEMOKRASIA NCHINI TANZANIA

Watanzania wengi wameweza kupatasomo la Demokrasia kupitia Kenya chini ya Rais wao Uhuru Kenyatta kwa kuwa muhumini mkubwa wa Demokrasia Barani Africa na watanzania wengi kumkumbuka Rais Mstaafu Kikwete kuwa aliweza kujaribu kusimamia Demokrasia nchini na kuweza kuleta maendeleo ambayo yameweza kuonekana katika taifa letu,

Watanzania wengi wanasema kenya imepiga hatua kimaendeleo ni kutokana na Demokrasia ambayo imeweza kusimamiwa na kuweza kufanikisha mataifa mbalimbali kuweza kuwekeza na kusaidia katika sekta mbalimbali kiuchumi mpaka kufikia hapo,

Tumeweza kuona kenya wameweza kusimamia Demokrasia katika uchaguzi wao pia wameweza kusimamia,

Watanzania wanasema kuwa Kikwete aliweza kujaribu ila akuweza kufikia viwango vya kenya katika Demokrasia ila Fundisho kwa Raisi wa sasa kuweza kusimamia Demokrasia nchini kama ana malengo makubwa ya maendelea maana demokrasia inaendana sawa na maendeleo katika taifa lolote hasa taifa letu ambalo ni kubwa hapa barani africa,

Wananchi wa Tanzania wanasema nchi yetu kwasasa demokrasia imeshindwa kusimamiwa kutokana na kiongozi wa juu wanchi kushindwa kusimamia hilo kwani Amna uhuru wa habari,uhuru wa kujieleza,kufanya mikutano ya kisiasa,kufanya maandamano mbalimbali nchini na mambo mbalimbali yameweza kuifanya tanzania kushuka kwenye viwango vya nchi ambazo zinaimani na demokrasia,

Watanzania wengi wanasema ndio maana maendeleo mengi yameweza kushuka katika nchi yetu katika sekta mbalimbali na katika jamii mbalimbali maisha yamekiuwa magumu sana pia wahisani nao wamekuwa njia panda kuweza kuwekeza nchini pia.

Wananchi wanasema mahakama inashindwa kufanya kazi kwa uhuru,bunge pia na vyombo vya usalama.

Maoni