BAADA YA SHEKH PONDA KUKAA NDANI SABABU KUONGEA KUHUSU LISSU SASA MH KIGAILA NAE YUPO NDANI.

Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo Mhe. Benson Kigaila anashikiliwa na Polisi katika kituo kikuu, Kanda Maalum ya Dar es salaam.

Mhe. Kigaila alifika kituoni hapo jana majira ya mchana akiitikia wito wa jeshi Polisi waliomtaka afike kwa mahojiano kuhusiana na kauli zake alizozitoa wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu shambulio la Mhe. Tundu Lissu.

Hata hivyo tangu alipofika akisindikizwa na Wakili Fred Kihwelo na kumaliza kumchukua maelezo walikataa kumwachia kwa maelezo kwamba anaetakiwa kuidhinisha dhamana hakuwepo.
Mapambano yanaendelea.

Maoni