WATANZANIA WACHEFUKA NA KAULI ZA MAGUFULI NA KUBAKI KUSHANGAA NI YEYE AU?

1. Kuna taasisi za umma zilikua zinafanyia mikutano ya bodi nje ya nchi. Wakiwa huko wanapandishiana mishahara hadi mil.40. Mimi mshahara wangu ni mil.9 tu kwa mwezi. Sasa nimezuia mikutano ya bodi kufanyika nje. Waliokua wananufaika hawawezi kunipenda. Lakini nikipendwa na mke wangu inatosha, sikuja Ikulu kuuza sura.
2. Watumishi waliokua na vyeti vya kughushi ndio wanaonitukana mitandaoni. Sibabaishwi. Nikiona najua hawa ndio wale 12,000 wa vyeti feki wanahangaika.
3. Makamu wa Rais amebakiza miezi miwili tu ahamie Dodoma. Mimi nitahamia mwakani. Halafu nione ambaye atabaki Dar es salaam. Atanieleza.
4. Nina taarifa kuna wakurugenzi watano wa halmashauri ni walevi. Hawa lazima nitawaondoa.
5. Sijapandisha mishahara ya watumishi na sitapandisha kwa sababu sikuchaguliwa kupandisha mishahara. Nilichaguliwa kusaidia wananchi wanyonge wapate huduma. Jukumu langu ni kutoa huduma kwa wananchi.
6. Makonda ni mchapakazi. Hata kama hajui kusoma hata herufi "A", lakini kwasababu anakamata madawa ya kulevya, basi huyo ni msomi mzuri sana.
7. Kama kuna diwani ambaye hana kazi ya kujiingizia kipato ajiuzulu udiwani haraka.!

Maoni