BILA MAADILI BORA NDANI YA NCHI YETU TAIFA HALITASONGA MBELE.
Pata kiungo
Facebook
X
Pinterest
Barua pepe
Programu Nyingine
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Suleiman Jaffo amesema kuwa
bila kusimamiwa kwa maadili katika jamii taifa litashindwa kusonga mbele
katika juhudi za kujenga jamii inayochukia rushwa.
Ameyasema hayo wakati akizindua Maadhimisho ya Maadili ya Kitaifa
Mjini Dodoma ambapo amewakemea viongozi wote wanaokumbatia rushwa na
kuziagiza mamlaka zinazosimamia maadili kuwachukulia hatua kali ili
kupunguza tatizo hilo nchini.
Kwa upande Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG, Prof.
Mussa Assad amesema kuwa taasisi hiyo inaendelea kusimamia maadili na
kupambana na rushwa pamoja na kusimamia maadili na haki za binadamu,
hivyo kuendelea kuboresha ufanisi kwa jitihada za serikali.
Hata hivyo, kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni wajibika piga
vita rushwa zingatia maadili haki za binadamu na utawala bora kuelekea
uchumi wa kati.
Maoni
Chapisha Maoni