BAADA YA TLS KUSEMA WANAGOMA POLISI WAMEKUJA NA MAJIBU HAYA NINI?KITAENDELEA KESHO

 
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es sallam limekanusha kuhusishwa na taarifa zilizozagaa kwenye vyombo ya habari kuhusu uvamizi na kulipua mabomu katika ofisi za wanasheria (IMA ADVOCATES)zilizopo upanga Dar es salaam 

Akitoa taarifa hizo mapema leo katika ofisi za polisi kanda hiyo ,Kamishna mwandamizi wa jeshi la polisi (SACO) Benedict Mtalika amesema uchunguzi wa awali uliofanyika umebaini kwamba usiku wa kuamkia tarehe 26/8/2016 majira ya saa 7 na saa 8 usiku watu wasiojulikana utambulisho wao na idadi kamili walifika katika ofisi hizo wakiwa namagari mawili huku wakijifanya ni maaskari wa polisi na kuwarubuni walinzi wa jengo hilo

Walinzi hao walichukuliwakwenye moja ya gari waliokuwa nalo ambapo baada walinzi hao walikutwa maeneo ya kawe wakiwa hawajitambui alisema Benedict Mtalika,

Aidha ameeleza kuwa kundi lililobakoi liliingia ndani ya ofisi hizo na kuweka milipuko iliyotengenezwa kienyejji ambayo baadae ililipuka kusababisha uharibifu wa mali na jengo laofisi hiyo pamoja na majengo ya jirani,

Amesemaji wa jeshi la polisi kanda maalumu linawahakikisha wananchi kuwa litaendelea kufanya uchunguzi wa awali ilikubaini watu hao waliofanya tukio hilo iliwafikishwe katika vyombo vya sheria,

Maoni