Mkuu
wa Kitengo cha Sheria Balaza la Taifa la usimamizi wa mazingira
Tanzania (NEMC), Manchale Heche akizungumza na wandishi wa habari
(hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juu ya zoezi la Bomoabomoa maeneo
ya miundombinu na maeneo yote hatarishi nakuwataka wananchi waliojenga
katika fukwe za bahari Kingo za mito na mikondo ya bahari kuhamisha mali
zao mapema.
Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Baraza la Taifa la Usimamizi
wa Mazingira (NEMC) na Manispaa za jiji la Dar es salaam zitafanya zoezi
la kuondoa wavamizi maeneo yote ya Mabondeni, kingo za mito na za
Bahari, maeneo ya wazi, maeneo ya miundombinu na maeneo yote hatarishi
zaidi ya 150 katika jiji la Dar es salaam. Bomoa bomoa ya leo
inaendelea katika Bonde la mto msimbazi.
Wananchi wanasema serikali inachukua nguvu kubwa sana katika bomoabomoa hiyo na kufanya watu kuishi kwa shida nyingi kwani wengi wao walijenga nyumba kwa kutumia mikopo.
Gari la Bomoabomoa katika maeneo ya msimbaziWatu wakitoa vitu kabla ya kubomolewa
Maoni
Chapisha Maoni