IGP SIRRO KAWEZA KUONGEA KUHUSU KUPATIKANA KWA BEN SAANANE

IGP SIRRO ambaye alikuwa katika kipindi cha dakika 45 kupitia kituo cha television cha ITV kikiwa chini ya SAM MAHELA na kuweza kuulizwa maswali mbalimbali ambayo yapo chini ya jeshi la polisi katika kusimamia usalama wa raia na mali zao hapa nchini,
IGP ameweza kusema swala la hari ya usalama hapa nchini linaendelea kuwa salama tofauti na vipindi vya nyuma na kupata sifa sehemu mbalimbali East Africa yote kutokana tumeweza kuimalika katika usalama wa nchi,
IGP ameweza kusema hari ya kibiti imekuwa sawa ingawa sio sana na kupinga kuhusu polisi inahusika katika mauwaji ya watu ambayo walikutwa kwenye viroba na kusema sio polisi ambao wameweza kuhusika kwa tukio hilo,
IGP ameweza kusema kamatakamata ya wapinzani itaendelea na hapa bado mbona maana kata mtu anavunja sheria za nchi lazima tumchukue tumwohoji na kama tutamkuta na tatizo basi tutaweza kumfungulia kesi  ila kama ana tatizo tutamwachia Je?wanaovunja sheria ni wapinzani tuningeweza kumuuliza endapo ningekuwa nae karibu,
SAM MAHELA: NAOMBA KUULIZA KUHUSU SWALA LA BEN SAANANE NI MDA MREFU POLISI MPO KIMYA WAZAZI WAKE WAPO KIMYA,WANANCHI WAPO KIMYA,CHAMA CHAKE KIPO KIMYA,UNAKIPI CHA KUWAAMBIA WATANZANIA MAANA MPAKA SASA NI MWAKA MZIMA

IGP SIRO: Kuhusu swala la ben saanane bado upelelezi unaendelea ila naomba kama kuna mtanzania ambaye anaweza kusaidia jeshi la polisi kuhusu kupatikana kwa kijana huyu tunaoba msaada kwa kutoa taarifa ila kikosi chetu ya upelelezi kinaendelea na kazi ya upelelezi

Nini maoni yako

Maoni