Katibu wa DRFA baada ya kuvamiwa na majambazi waliodai 150 Milioni


Mchana wa jana August 29, 2017 zimeenea taarifa kwamba, watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamevamia ofisi za Chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) wakidai wapewe shilingi milioni 150 ambazo wanaeleza zilikuwepo kwenye ofisi hizo maeneo ya Karume (Machinga Complex).
Katibu wa DRFA Daudi Kanuti ameelezea sakata zima lilivyokuwa kuhusu uvamizi huo ambao ulitokea saa 4 asubuni, hadi wakati Kanuti anazungumza bado hakukuwa na mtuhumiwa yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio ambalo liliripotiwa kwenye kituo cha polisi Msimbazi.
Wakati jana naingia ofisini nilikutana na jamaa mlangoni kwa secretary wetu akaniuliza wewe ndio Kanuti nikamjibu ndio, akasema pandisha ngazi twende juu nikauliza kuna nini? Akasema panda tu usifanye chochote, nikagundua kwamba kuna hatari, nilipofika juu nikakuta wenzangu wawili wamefungwa kamba,” Daudi Kanuzi-Katibu DRFA.”
“Nikaniambia kaa hapo usifanye chochote, nikafungwa pingu halafu wenyewe wakatoka walivyorudi walikuwa na kamba na pingu wakanifunga mikono na miguu na wakaniweka plasta mfomoni. Wakaniambia sisi shida yetu ni pesa hapa kuna milioni 150 tunaitaka hiyo pesa.”

 “Wakanisachi mfukoni wakakuta funguo wakachukua, wakachukua simu ndogo pamoja na 200,000 ilikuwa mfukoni. Wakaanza kuingia kwenye ofisi kupekua, baadae nilivyorudi kuangalia nikakuta 450,000 iliyokuwepo ofisini imechukuliwa.”
“Mimi sikuona silaha lakini mwenzetu mmoja anasema alivyokamatwa alioneshwa silaha, mimi niliona mmoja wao akiwa na radio call pamoja na pingu. Hakuna mtu yeyote kati yetu ambaye alipigwa wala kuumizwa kutokana na tukio hilo. Tuliokolewa na jamaa zetu wa hapa ambapo baada ya hao jamaa kuondoka waliingia wakatufungua kamba.”

Maoni