KENYA YATOA SOMO LA DEMOKRASIA BARANI AFRICA BADO MASAA 24 YA MAHAKAMA KUTOA MAJIBU.

Mahakama ya juu kabisa nchini Kenya inasubiriwa kutoa uamuzi katika muda wa saa 24 zijazo kuhusu kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais. Kesi hii imekuwa ikisikilizwa tangu mwanzoni mwa wiki na jopo la majaji 7. Kesi hii ilifunguliwa na wanasiasa wa muungano wa upinzani wa NASA, wakidai kuwa ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta ulitokana na hila zilizofanywa kupitia mfumo wa computer wa tume ya uchaguzi IEBC na wanataka matokeo hayo yafutwe na uchaguzi kuitishwa upya ndani ya siku 60. Kwa upande wa pili tume ya uchaguzi IEBC na mawakili wa chama cha Jubilee wanasisitiza hakuna ushahidi wa kuyafutilia mbali matokeo ya uchaguzi yaliyompa rais Uhuru Kenyatta ushindi. 
Jee kipi kinaweza kutokea pale majaji watakapoikata kauli yao?

Maoni