Mahujaji Waendelea ibada ya Hijja Mjini Makka 2017

Zaidi ya Mahujaji milioni mbili wa Kiislamu kutoka duniani kote Jana Jumatano wanaanza ibada ya Hijja katika maeneo matakatifu ya Makka na Madina ikiwa ni nguzo kuu kwa kila muislamu kuitimiza katika maisha yake.


Hii ni moja ya nguzo kuu za kidini ambayo kila Muislamu anapaswa kuitekeza angalau mara moja katika maisha yake ikiwa anao uwezo wa kufanya hivyo. Mwanzoni mwa Hajji leo, mahujaji walianza kwa kuzunguka nyumba ya mwenyezi Mungu ya Kaaba mjini Makka na kutekeleza ibada zinazoaminika kufuatilia nyayo za Mitume Ibrahim na Ismail.
Zaidi ya mahujaji milioni mbili wanashiriki ibadi hii kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na mamla za Saudia, idadi hii ikiwa ni zaidi ya waliohudhuria Hajji ya mwaka jana waliokadiriwa kufika milioni 1.8 na elfu 24,000 mwaka 1941. Afisa mmoja wa Indonesia ameliambia gazeti la Saudia kwamba jumla ya Mahujaji 221,000 kutoka Indonesia tayari wamefika mjini Makka ikiwa ndiyo idadi kubwa kutoka nje ya nchi.
Haddsch Islamische Pilgerfahrt nach Mekka | Kabaa, Große Moschee (picture-alliance/AP Photo/K. Hamra)  Mahujaji mjini Makka wakigusa nyumba ya mwenyezi Mungu Kaaba

Hali ya usalama 
Wizara ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia inasema imesambaza maafisa wa usalama zaidi ya 100,000 ili kuhakikisha usalama. Walinzi wengine wa kiraia elfu 17,000 wakisaidiwa na magari karibu 3000 wanasaidia kulinda usalama. Msemaji wa wizara hiyo Meja Jenerali Mansour Al-Turki amesema, "kwa kawaida tunakuwa na idadi ile ile ya vikosi vya usalama wakati wa Hajji na idadi inaongezeka na kupita 100,000, wanachama wamegawanyika katika majukumu tofauti ili kulinda usalama. Kwa kila afisa usalama ana majukumu mawili, Moja ni kumlinda hujaji na pili ni mpango unaohusiana na kila mtu anachopaswa kuetekeleza katika eneo hili."
Pamoja na hilo, Saudi Arabia imeweka maelfu ya kamera za usalama katika njia watakazopita mahujaji huku maelfu ya mabanda yaliyo na viyoyozi yakiwekwa katika eneo la Mina kati ya mlima Arafat na Makka ili kuwahifadhi mahujaji. Shirika la Hilali nyekundi la Saudia pia limeongeza wafanyakazi wa ziada 2,468 pamoja na wale wa kujitolea takribani 500 ambao watafanya kazi na magari 326 ya kubebea wagonjwa na helikopta nane.
Saudi Arabien | Muslimische Gläubige beten in der Pilgerstätte Mekka (picture-alliance/AP) Mahujaji wa Kiislamu wakiswali katika msikiti mkuu kabla ya kuanza kwa Hajji
Kwa mujibu wa taarifa za habari za nchini humo zaidi ya wapishi 700 wameajiriwa ili kuwahudumia waumini hao. Saudi Arabia ina matumaini ya kuwakaribisha mahujaji milioni 30 kwa mwaka hadi kufikia 2030 katika ibada mbalimbali za Hajji. Mmoja wa Mahujaji kutoka Misri Ahmed Ali anasema, "asanteni nyote, kama mnavyojua ni hisia zisizoelezeka, ni Hajji yangu ya kwanza na namshukuru Allah. Kila kitu kiko sawa. haielezeki, ni hisia za kiroho. Asante Allah najisikia vizuri."
Mgogoro wa kidiplomasia
Hijja ya mwaka huu inashuhudia mahujaji wa Kishia kutoka Iran wakirejea kufuatia mgogoro wa  kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Kiislamu na hasimu wake wa Kisunni Saudi Arabia. Pia inakuja wakati ukanda wa Ghuba ukigubikwa na mgogoro wa kisiasa na makundi ya wanajihadi wa Kiislamu wakikabiliwa na mbinyo nchini Syria na Iraq.
Mamlaka za Saudi Arabia zimewekeza pakubwa kuhakikisha kwamba mauaji ya 2015 yaliyopelekea watu karibu 2300 kupoteza maisha wakiwemo Wairan 464, hayajirudii.
Riyadh na Tehran zilikata mahusiano miezi michache baadae, baada ya hukumu ya kifo dhidi ya mhubiri wa kishia nchini Saudi Arabia na kuchochea mashambulizi katika balozi za Saudi nchini Iran.
Hajji hiyo pia inaanza katikati mwa mgogoro wa kidilpmasia kati ya mataifa kadhaa ya kiarabu na Qatar inayotuhumiwa kwa kuyafadhili makundi yenye itikadi kali na kwa kuwa karibu na mpinzani mkuu wa Riyadh yani Tehran.

Maoni