RAIS MSTAAFU KARUME AMEWEZA KUTOA POLE KUTOKEA MLIPUKO IMMA ADVOCATE ILA MWANASHERIA WA SERIKALI,KAIMU JAJI KIMYA MPAKA LEO.

Kituo cha sheria na haki za binadamu pamoja na rais wa chama cha wanansheria Tanganyika wamemtaka rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania kuteua jaji mkuu mara moja ili aweze kusimamia shughuli za mahakama kwa mujibu wa sheria. Hayo wameyazungumza katika mkutano na waandishi wa habari, na kuongeza kuwa kaimu jaji mkuu lazima atoe tamko la kulaani shambulio hilo ambalo wamelitaja si la kwanza kutokea likianziwa na lile la ofisi za rais wa chama cha mawakili Zanzibar zilizoshambuliwa mwaka uliopita.

Pia wameweza kulani vikali kwa tukio ambalo limeweza kutokea katika jengo la Imma advocates na kupinga vikali na Fatuma Karume ameweza kusema kuwa sijui kama wanaweza kumpata ambaye amefanya matukio hayo kwana tumeweza kuona matukio mengi yanaendelea hapa nchini ila wahusika awapatikani na kuweza kuchukuliwa hatua na kusema kuwa baba yake Rais mstaafu wa zanzibar mzee karume ameweza kutoa pole kwa tukio hilo

Pia ameweza kuwashanga viongozi kama mwanasheria wa serikali,kaimu jaji mkuu na waziri wa sheria wameshindwa kupaza sauti na wala kutoa pole kwa wanasheria hao na kusema anamwachia mungu na mungu ataweza kutoa hukumu kwa wote ambao wameweza kutenda hayo,

Ameweza kusistiza kuwa watanzania tunatakiwa kuunga kwenye shida na raha itikadi za vyama zisitufanye tuwe maadui hapo tutakuwa tunalipeleka taifa letu pabaya,

Maoni