Wakili Fatuma Karume katokwa machozi na kuwalaumu Waziri wa sheria na katiba,Jaji mkuu na Mwanasheria mkuu wa serikali kwa ukimya



Wakili Fatuma karume katoa lawama kwa waziri wa sheria,Mwanasheria mkuu wa serikali na jaji mkuu kukaa kimya mpaka sasakuhusu kuvamiwa kwa jengo la mawakili la Imma Advocate na kupigwa na mabomu mpaka kufanya matatizomakubwa ya jengo pamoja na mali ambazo zipo ndani ya jengo ikiwemo kazi za wateja wao,

Ameweza kutoa lawama kwa polisi kwani wanashindwa kutoa ushirikiano na wahusika katika ofisi hiyo na kusababisha kuumia zaidi juu ya tukio hilo alikuwa akitoa maelezo hayo akiwa analia,
Wakili Fatuma Karume kasema kuwa tulitegemea kuona wanasheria mkuu au waziri wa sheria wakisimama na kukemea vikali juu ya tukio hil ila mpaka sasa wapo kimya na amna neon lolote ambalo wamesema ni kitu cha kufezehesha sana,
Tukishindwa kukemea tendo hili na kuchukua hatua kali kwa wahusika tutegemee kuona matendo mengi kama haya kuendelea kutokea hapa nchini,

Uongozi wa Uws Media unafanya jitihada kuweza kumtafuta waziri wa sheria na jaji mkuu tuone nao wanatamko gani?juu ya tukio hili,
Tutaendelea kuwapa habari kupitia chombo chetu cha habari Uws Media.
SOURCE: #UWS #MEDIA

Maoni