Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesema
limepunguza mgao wa chakula cha misaada kwa wakimbizi 320,000 wanaoishi
kaskazini magharibi mwa Tanzania kutokana na uhaba wa fedha kutoka kwa
wafadhili. Katika taarifa iliyoitoa leo, WFP imesema inahitaji kwa
dharura kiasi cha dola milioni 23.6 kuweza kukidhi mahitaji ya chakula
cha wakimbizi hadi mwezi Desemba. Wakimbizi hao ni kutoka Burundi na
CongoMwakilishi wa WFP nchini Tanzania Michael Dunford amesema mgao wa
chakula utazidi kupunguzwa iwapo wafadhili hawatatoa misaada mara moja.
Umoja wa Mataifa umekuwa pia ukiwaomba wafadhili kuwasaidia zaidi ya
wakimbizi milioni mbili wa Sudan Kusini walioko katika nchi jirani.
Maoni
Chapisha Maoni