Wananchi Wa Jimbo La Iringa Mjini Wanasema Bado Wanaimani Kubwa Na Msigwa

Katika mazungumzo baadhi ya wananchi wa iringa wanasema kuwa bado wanaimani kubwa na mbunge wao ingawa kuna watu wanatokea na kutaka kumchonganisha  mbunge na wananchi wake ila wananchi wamesema atuwezi kuskia la mtu maana Mh Mbunge Msigwa kaweza kuwatetea vyema kama bunge na Tanzania ndani ya bunge na nje ya bunge,

Siku kazaa zimepita kulikuwa na majibishano katika mitandao ya kijamii na katbu mwenezi wa ccm,

Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa ameibuka na kumjibu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole na kumwambia kuwa hana uwezo wa kumuondoa kwenye jimbo la Iringa Mjini 2020 kama alivyoahidi.Mchungaji Msingwa amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kumtaka Humphrey PolePole kuwauliza wenzake ambao walimtangulia katika nafasi yake hiyo ya Uenezi kuwa watampa majibu.

"PolePole huna uwezo huo waulize wenzio waliokutangulia , mimi sijateuliwa kama wewe"alisema Mchungaji Msingwa

Siku mbili zilizopita Mchungaji Msigwa alisema kitendo cha Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma kusema anamkumbuka Mbunge wa Mtama Mhe. Nape Nnauye ni ishara kuwa Humphery PolePole ameshindwa kuvaa vizuri kiatu alichoachiwa kama Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, ndipo hapo PolePole alipokuja na kumwambia Msigwa kuwa huu ni wakati wake wa mwisho kama Mbunge wa Iringa Mjini.

"Kitu kimoja nakuahidi, hii ni 'term' yako ya mwisho, tunakurudisha kufanya kazi ya Uchungaji maana naona Mchungaji anajichanganya na mbuzi" alisema Humphery PolePole

Hata hivyo siku moja baada ya ahadi ya Humphery PolePole madiwani watatu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Iringa Mjini walitangaza kujiuzulu nafasi zao kwa kile walichodai kuwa viongozi wa juu wa chama hicho Iringa wamekuwa wakiwatenga na kuwatuhumu kuwa ni wasaliti, hivyo wameamua kujiuzulu nafasi zao kama madiwani.