BAADA YA KUKAMATWA KWA BOMBADIER SASA WALE WACHINA WALIOKAMATWA NA SAMAKI SASA WAMKALIA KOONI MAGUFULI,SASA WANADAI CHAO
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeamuru Serikali ya Tanzania kulipa meli ya uvuvi pamoja na samaki
waliokamatwa miaka mitano iliyopita mali
ya raia wa China,
vyote vikiwa na thamani ya Dola za Marekani milioni 3.2.
Mahakama hiyo imetoa amri hiyo baada ya kuwaachia washtakiwa
wawili raia wa China, Hsu
Tai na Zhao Hanquing, waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya kuvua samaki katika
Ukanda wa Kiuchumi wa Bahari ya Tanzania
bila kibali, maarufu ‘Samaki wa Magufuli’.
Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana, Wakili wa
Utetezi, Kapteni Ibrahim Bendera, alisema meli iliyokamatwa na wateja wake
ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani milioni 2.5 na samaki waliokutwa nao
walikuwa na thamani ya Dola za Marekani 720,000.
“Bado tunasubiri maelekezo ya wamiliki wa hiyo meli kuhusu
hatua za kisheria zinazostahili ili wapate fedha hizo” alisema Kapteni Bendera
kwa njia ya simu.
Agosti 22, mwaka huu, Hakimu Mkazi Mkuu, Mfawidhi, Isaya
Arufani, alisoma uamuzi wa kuwaachia huru Wachina hao, pamoja na mambo mengine,
aliamuru serikali kulipa mali hizo pamoja na hati zao za kusafiria.
Kesi hiyo awali ilikuwa ikiwakabili watu 38 kutoka mataifa
tofauti ya Bara la Asia ya China,
Ufilipino, Vietnam
na wawili raia wa Kenya.
Walikamatwa Machi 8, mwaka 2009 wakivua na walikutwa na tani
293 za samaki, wakati huo, Dk, John Magufuli akiwa Waziri wa Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi.
Kati ya washtakiwa hao, mmoja alifariki dunia, wengine 35
waliachiwa huru na wawili kutiwa hatiani.
Maoni
Chapisha Maoni