Asubuhi ya leo trh 24/09/2017 wabunge wawili wa Arusha ambao ni mhe.JOSHUA NASSARY na mhe.GODBLESS LEMA wamezungumza na waandishi wa habari kwa ajili ya kuutarifu umma ya uchafu uliofanyika na CCM kupitia serikali hii ya awamu ya tano kwa madiwani tunaoaminishwa kuwa wameamua kuachia udiwani wao na kumuunga mkono rais (hapa watu walijiuliza, kwanini ni Arusha tu?)
Mhe.Nassary amesema amefanya uchunguzi kwa muda wa miezi minne huku akitumia vifaa vya kisayansi kutoka Uingereza, na kubaini rushwa ilivyotumika kuwanunua madiwani hao.
Mhe.Nassary amesema kama kweli rais anaipinga rushwa, basi aruhusu Nassary ampelekee ushahidi huo usiokuwa na shaka.
Pia, mhe.Nassary ameomba kuwasilisha ushahidi huo kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, IGP,Mkurugenzi wa makosa ya jinai, na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (TISS).
Pia, mhe.Nassary ameomba kuwasilisha ushahidi huo kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, IGP,Mkurugenzi wa makosa ya jinai, na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (TISS).
Mhe. Nassary ameahidi kuwa, endapo ushahidi huo hautakuwa wa kweli, ameahidi kwa kinywa chake mwenyewe kuwa atakuwa tayari kujiuzuru Ubunge wake.
Kwa mujibu wa ushahidi, mambo yote hayo yameratibiwa ndani ya Ofisi za umma.
Kwa mujibu wa ushahidi, mambo yote hayo yameratibiwa ndani ya Ofisi za umma.
Hapa ngoma imefika patamu,maigizo ya CCM na serikali yake mwaka huu yamegonga mwamba. CHADEMA inao vijana makini sana na wanaofanya mambo kwa weledi mkubwa.
Tunamsubiri Rais akubali kupokea hii taarifa ya ushahidi wa rushwa, ikiwa kweli ameamua kuzuia rushwa!!
Tunamsubiri Rais akubali kupokea hii taarifa ya ushahidi wa rushwa, ikiwa kweli ameamua kuzuia rushwa!!
Maoni
Chapisha Maoni