CCM WAMEONDOA IMANI NA MAGUFULI SASA WAMTAKA MEMBE 2020.

CCM YA MAGUFULI HALI SI SHWARI
Team Bernard Membe waja Juu.
"Sisi wana-CCM tulikuwa na matarajio makubwa sana kwa Magufuli maana tulijua kwamba sasa tumempata Rais wa wanyonge, viwanda vitajengwa, ajira zitapatikana, uchumi utakua, Zahanati zitajengwa kila Kijiji, Vituo vya afya kila Kata, Dawa zitapatikana kwa wingi mahospitalini, kero ya maji itaisha kabisa na hata ile ahadi ya millioni 50 za kila Kijiji tulijua zitatoka mapema sana akiingia Ikulu".
"Badala yake tumeambulia maneno mengi kila siku kwenye hotuba zenye hasira, chuki na fitina, tumeambulia watanzania wenzetu kutekwa, kuuawa, wenzetu kukamatwa ovyo, kutishiwa silaha za moto hata baadhi yao kujeruhiwa na silaha hizo za moto wazi wazi tena mchana kweupe, bomoa bomoa za kuwakomoa baadhi ya watu, bunge kuzuiliwa live, vyakula bei ghali, ajira hakuna na kibaya zaidi, hata viongozi waliojenga chama kama Kinana, Nape n.k hawathaminiwi tena. Uzalendo ni wa maneno tu, wauaji ndio wazalendo".
Bernad Membe anatosha #2020.

Maoni