DKT LWAITAMA TANZANIA AIWEZI KUWA NA KAULI KUTOKA KWA MTU MMOJA WAKATI NI NCHI YA KIDEMOKRASIA.

Dkt Lwaitama adai kuwa msingi ya uongozi imepotea kabisa toka tutoke katika mfumo wa ujamaa na kwenda kwenye ubepari ambapo sasa ndio tupo maana ubepari ni mbaya sana katika taifa changa kimaendeleo kama hili,
Dkt Lwaitama amesema misingi ya uongozi kwasasa amna kabisa kwani hari ambayo ipo kwasasa ni kunyonyana wajuu anamnyonya wa chini kwahiyo amna maendeleo hapo,

Pia ameweza kueleza kuwa nchi kwasasa aipo huru kwani vyombo husika vinashindwa kusimama na kutenda kazi kwa haki kutokana na mfumo wa katika na kufanya kazi kwa hofu ya kumwogopa mtu na kusema Mahakama aipo huru,Bunge alipo huru, Vyombo vya Dora pia avipo huru kabisa katika kusimamia kazi zao na kusubiri Oda kutoka juu,

Demokrasia kwasasa katika nchi hii imeshindwa kusimamiwa maana tunaskia kauli ya mtu mmoja na sio kauli za watanzania kutoa maoni yao inaonekana ukitoa maoni kwasasa inakuwa ni tatizo wakati nchi yetu yaa kidemokrasia hapo ndipo nashangaa wakati nchi nyingi zimepiga hatua ni kutokana na kusimamia Demokrasia katika mataifa yao,

Nchi yetu kwasasa tunaskia kauli ya mtu mmoja ambayo ni tatizo sana katika kutafuta maendeleo ya taifa letu kwani wananchi wakiweza kuwa huru wanaweza wanaweza kueleza hisia zao na viongozi kupokea na kuweza kufanyia kazi pia,

Angalia nchi inaenda wapi?kama mikutano ya kisiasa imeweza kuzuiwa na mtu mmoja na tunasema tunataka maendeleo wakati katika mikutano ya kisiasa hao ni watanzania waweze kueleza mambo mbalimbali ndani ya taifa lao nawe kama kiongozi wa juu kuweza kusimamia sasa kuna hofu ya nini?

Kwasasa Taifa letu linatakiwa kupata rasimu ya katiba ya jaji warioba ili kuweza kupunguza baadhi ya kazi za viongozi wetu wa juu ili waweze kutumikia wananchi bila kuwa na hofu ya mtu flani maana wengi wanafanya kazi wakiwa na hofu na watu frani wanaweza kuwaachisha kazi zao,

DKT Lwaitama kaweza kusisitiza katiba mpya ni muhimu sana kwasasa maana tumeweza kujifunza zaidi kwa wenzetu na Raisi wetu wa nchi awezi kusema anataka kuweka taifa letu sawa alafu akasema katiba sio kipaumbele chake hapo atakuwa anakosea sana na hayo maendeleo sijui kama yanawezakupatikana bila katiba mpya.

Katiba Katiba Katiba.
Source Eatv


UWS MEDIA

Maoni