JAJI MKUU WA TANZANIA ATAWEZA KUFATA NYAYO ZA MAJAJI WA KENYA KATIKA KUSIMAMIA HAKI ZA WANANCHI,TUTONE KWA MH LISSU.
September 21 2017 Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amekutana na vyombo vya habari kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe rasmi kwenye nafasi hiyo.
Jaji Mkuu ameitoa taarifa kuhusu mkutano wa chama cha mahakimu na majaji wa jumuiya ya madola utakaofanyika katika ukumbi wa benki kuu kuanzia tarrehe 25-27/9/2017.
Moja ya swali ambalo ameulizwa na wanahabari ni kuhusu ishu ya Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi na amesema haya ana akaweza kujibu
Tukio hilo ni la kihalifu , uhalifu Mkubwa ni jaribio la kuua na kitu cha kwanza ni kukusanya ushahidi na huo ushahidi utakusanywa hapa hapa Tanzania, asikudanye mtu kwamba mtu atatoka nje atakuwa na uwezo wa kukusanya ushahidi’
Jaji Mkuu ameweza kusema basi waandishi na watanzania tuwe tayari kuweza kusubiri uchunguzi wakati mambo mengine yakiendelea kufanyiwa kazi na wahusika bila kuingiliwa na mtu yoyote yule.
Maoni yako Mhimu
JibuFuta