KAULI YA MH LISSU KWA MH ZITTO TUMESHINDA NA TUNAENDA KUWASHINDA NIMEFIKA HAPA BAADA YA KUWABANA KILA KONA.

Mwisho wa wiki hii iliyomalizika nilikuwa Nairobi kwaajili ya kumsabahi ndugu yetu Tundu Lissu, siku mbili hizi za kumuona Lissu kitandani pale zimeniacha nikifikiria sana. Nimerudi nchini nikiwa mwenye unyenyekevu zaidi kwasababu ya nguvu na ujasiri ambao ndugu yangu ameuonyesha licha ya kuwa kwenye maumivu makali.
Si mara nyingi hapa nchini utasikia tukiongelea ujasiri. Lakini namfikiria Lissu na vile nilivyojisikia nikiwa pamoja naye Nairobi. Najua hivyo ndivyo alivyo. Waliomshambulia wamemuumiza. Wamemuumiza kweli. Na bado wakati tuliokuwa naye amenionyesha shukrani, ari na pia ucheshi. Huo ni ujasiri.
Alichopitia na anachoendelea kupitia Lissu sio kitu rahisi kwa mtu yoyote kutafakari. Kufikiria hali ile kungeniacha nimeumia moyo Sana kama asingesema maneno haya kwangu; "Tumeshinda, Tumeshashinda".
Ujasiri ni Lissu
Kabwe Z. Ruyagwa ZittoKiongozi wa Chama - ACT Wazalendo
Septemba 18, 2017

Maoni