KAULI ZA JAKAYA KIKWETE ZIMEKUWA ZA KISHUJAA NA FUNDISHO KWA SERIKALI YA AWAMU TANO CHINI YA MAGUFULI.

KUMBUKA USHAURI WA KIKWETE KWA WANACCM
Mwaka 2012 akiwa mwenyekiti wa chama hicho, Rais mstaafu, Jakaya Kikwete alitoa ushauri muhimu kwa CCM ili iweze kuimarika. Aliitaka iache kubweteka na kuwategemea polisi katika masuala ya kisiasa.
Katika ushauri huo, Kikwete alisema kitendo cha CCM kuitegemea polisi ni kujidanganya na kimepitwa na wakati.
Mnaishia kulalamika tu kila siku, eti wanatukana halafu mnaishia kusema ndiyo kawaida yao au utasikia mtu anasema eti Serikali haipo! Kazi ya Serikali siyo hiyo, hiyo ni kazi ya kisiasa maana hao ndio wenzenu"
Sasa mnataka wakisema Serikali ya CCM haijafanya kitu polisi wawafuate au wakisema Kikwete nchi imemshinda polisi wawakamate? Kama wakisema hatujafanya kitu ni kazi yenu kusema kwamba tumefanya kitu, waonyesheni barabara, shule na mambo mengine,”
Jakaya Kikwete: Novemba 13, 2012, siku mbili baada ya kuchaguliwa mara ya pili kuwa mwenyekiti wa CCM.
Huku akirudia mara kadhaa maneno hayo alisema, “Nataka mfahamu ndugu zangu kuwa tukiishi kwa kutegemea Jeshi la Polisi kufanikisha mambo yetu, tutakwisha na tutakwisha kweli.!
Hekima ni heri kuliko Ubabe!

Maoni