Rais Uhuru kenyatta, akihutubia taifa, amewahimiza Wakenya kudumisha amani.
"Jirani yako atasalia kuwa jirani, bila kujali mrengo wao wa kisiasa, dini, rangi".
Amesema hakubaliani na uamuzi uliotolewa na mahakama, lakini anaukubali.
"Watu hao sita (majaji) wameamua kwamba wataenda kinyume na mapenzi ya watu. Nyinyi Wakenya mlichagua wabunge wengi wa Jubilee, maseneta wengi wa Jubilee na wawakilishi wa wanawake wa Jubilee, wawakilishi wengi wa wadi wa Jubilee," amesema.
"Tuko tayari kurudi tena kwa wananchi, tukiwa na ajenda ile ile tuliyowasilisha, ajenda ya kuunganisha nchi. Kuunda chama cha taifa. Kuendeleza nchi hii.
"Hatuko kwenye vita na ndugu zetu wa upinzani.
"Tuko tayari kurudi kwa debe, kuongea na Wakenya, kuwaambia yale tunataka na yale tunataka kutenda."
"Watu wachache, watu sita, hawawezi kubadilisha nia ya Wakenya milioni 40. Wakenya ndio wataamua, na hivyo ndivyo demokrasia ilivyo."
Maoni
Chapisha Maoni