KESHO NI IJUMAA YA ALBADIR WAHUSIKA WA TUKIO LA MH LISSU WAJIANDAE KISAIKOLOJIA KAMA WAO WALIVYOPANGA SHAMBULIZI.

Kesho waislamu nchini watasoma dua ya Albadir kwa wote waliohusika na shambulio la risasi kwa Mhe.Tundu Lissu. Mikoa iliyodhibitisha kusoma dua hiyo ni Tanga, Mtwara, Lindi, Kaskazini Pemba, Kusini Pemba, Mjini Magharibi, Kilimanjaro, na Kigoma. Sheikh Anwar Mohamed wa Muheza atakayeongoza dua hiyo kwa mkoa wa Tanga amesema wamenuia madhara yawapate wote waliohusika, watoto wao, wajukuu zao, na ukoo mzima.
Ameeleza kuwa hawategemei dua hiyo kuzuiwa na Polisi kwa sababu wanafanyia ndani kama ibada nyingine. "Hakuna sheria ya kuzuia watu kuswali, lakini kama Polisi watajaribu kuzuia basi nao tutawaunganisha kwenye dua hiyo" amesema Sheikh Anwar.

Siku ya kesho ni siku ya mungu kujibu majibu yetu pembe zote za nchi.maoni ya watanzania






Maoni