MAKAMBAKO WAGOMA KUTUMIA EFD WATAKA AHADI YA MAGUFULI 2015 YA KUGAWA BURE ITIMIE

Wafanyabiashara wa mji makambako wakiongea na mkuu Wa mkoa wa njombe baada ya wafanyabiashara kugoma kufungua maduka wakilalamikia machine ya efd. 

Wafanyabiashara wamemwambia mkuu Wa mkoa wa njombe. Kuwa rais kipindi cha kampeni aliahidi kugawa machine za efd bure kwa wafanyabiashara. Hivyo wanamuomba Rais awagawawie hizo machine za efd ili wazitumie kama alivyoahidi kipindi cha kampeni

Wafanya biashara ambao wameweza kufanya magomo pia wamesema kuwa uchumi wa nchi unapolomoka kwa kiwango kuikubwa sana na tunatakiwa kununua kifaa hicho wakati hari ya maisha duni na raisi alisema kuwa yeye ni rais wa wanyonge ni vyema akasimamia kauli zake ambazo ameweza kusema mwenyewe katika kampeni inatakiwa aweze kuzitimia 

Pia wamesema wanataka kuskia kauli ya raisi mwenyewe juu ya hizo mashine,



Maoni