MANENO YA WATANZANIA JUU YA KUPIGWA KWA RISASI 20 RAIS WA TLS MH TUNDU LISSU.

-Sijawahi ichukia nchi yangu. 
-Sijawahi isemea wala kuinenea mabaya nchi yangu.
Leo ninaitazama nchi yangu kwa jicho la utofauti kabisa. Tumejisifu, tumejigamba na kuieleza dunia yakuwa sisi ni nchi ya amani na utulivu.
Tumejitolea mifano mingi sana. Tukijitanabaisha ya kuwa, sisi sio kama hao wala wale. Sisi ni bora zaidi kuliko maana tuna amani.
Tukasahau kabisa ya kuwa, matendo huongea zaidi kuliko maneno.
Kama nilivyo sema awali. Sijawahi wazia wala kuinenea nchi yangu mabaya. Ila kwa hiki, sina budi kusema ya kuwa. Tunajiongopea.
Tukio hili ni doa kubwa sana kwa Tanzania nje na ndani ya mipaka ya Tanzania.
Tuna wajibu wa kujitazama kwa kina.
Maana leo ni hali hii, kesho itakuwaje?

Maoni