MAONI YA MWANAHARAKATI MALISSA JUU YA RIPOTI YA ALMASI NA TANZANITE LEO BUNGENI

Nimesikiliza ripoti mbili za Kamati Teule za Bunge kuhusu Madini ya Tanzanite na Almasi, nimesikitika sana. Kamati ya Almasi imeongozwa na Mhe.Mussa Azan Zungu na ile ya Tanzanite imeongozwa na Mhe.Doto Biteko. Aisee hii nchi imeharibiwa sana.
Machache yaliyoelezwa;
1. Mwenyekiti wa kamati maalum ya Makinikia Profesa Abdulkarim Mruma, ambaye alieleza kwa uchungu namna nchi ilivyoibiwa kwenye dhahabu, kumbe nae ameshiriki kuiibia nchi kwenye Tanzanite na Almasi. Sijui kama unaelewa. Ni kwamba Prof.Mruma aliyedai kuumizwa na wizi wa dhahabu na yeye ameshiriki kwenye wizi wa Tanzanite na Almasi.
Kamati ya Biteko na ile ya Zungu zimempata Prof.Mruma na hatia ya kuruhusu madini ya Tanzanite na Almasi yapotee kizembe wakati akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya ukaguzi wa madini nchini. Profesa Mruma alipohojiwa aliiambia kamati kwamba alisaini bila kusoma documents. Alipoulizwa kwanini alisaini bila kusoma, alisema alikuwa 'busy' sana na hivyo hakupata muda wa kusoma documents na hivyo aliamua kusaini kwa kuwa aliwaamini watendaji wa wizara.
Imagine ni Prof.Mruma huyuhuyu wa kamati ya makinikia. Duuh.!! Aisee usimuamini mtu. Sasa alipata wapi ujasiri wa kukemea wizi wa dhahabu kama na yeye ameshiriki kuipa nchi hasara kwenye Tanzanite na Almasi? Na kwanini Rais alimteua mtu mchafu kuchunguza uchafu mwingine? Unawezaje kumteua mwizi wa magari akakamate wezi wa bajaj?
2. Ukishangaa ya Prof.Mruma utayaona ya Simbachawene. Kamati zote mbili zimempata Simbachawene na hatia ya kusaini Mikataba yenye madudu mengi yaliyoingiza nchi kwenye hasara kubwa. Simbachawene ni moja ya watu waliofanya STAMICO iwe ICU leo.
3. Mkataba wa madini ya almasi uliandaliwa nje ya nchi. Jaji Werema aliyekua Mwanasheria mkuu wakati huo, ameiambia Kamati kuwa aliagizwa kusaini Mkataba kabla ya kuusoma. Can you imagine??
4. Waziri Muhongo aliingia ofisini mwaka 2012 kwa mara ya kwanza kama Waziri wa Nishati na madini. Lakini akasaini leseni za uchimbaji wa tanzanite retrospectively. Yani akarudisha nyuma miaka miwili then akasaini. Yani leseni za mwaka 2010 zinaonesha zimesainiwa na Muhongo, wakati huo bado hajawa Waziri. Kumbe aliubackdate makusudi ili makampuni ya kigeni yanayochimba tanzanite yaweze kufidia gharama zao walizotumia wakati wakifanya tafiti.
5. Makampuni mengi ya kigeni yanayochimba madini ya tanzanite na almasi hayajasajiliwa nchini. Yamesajiliwa katika nchi yanakotoka, lakini hapa nchini hayajasajiliwa BRELA. Hayatambuliki. Lakini yana operate. Can u imagine??
Aisee, nimegundua kazi ya kulinda rasilimali za nchi hii ni ngumu sana. Anayejifanya kulinda huku, kumbe anaiba kule. What a shame.!!


Maoni