MCH MSIGWA AFUNGUKA MAZITO JUU YA UTAWALA WA NGUVU CHINI YA MAGUFULI.

Niliwahi kusema kuwa CCM ni weupe sana. Vyombo vya dola vikikaa pembeni CCM ni weupe kama karatasi.
Msigwa siyo mbunge wa Jimbo tu bali ni mbunge wa kitaifa. Taifa linahitaji watu aina ya Msigwa. Wabunge wa kitaifa wanaogopwa sana. Mkutano wake wa kata walijaa almost top police officers wa Mkoa na wilaya.
Akihutubia mbunge wa kalenga huwa anatumwa auxiliary police.
Polisi wamewasaidia tena CCM kuzuia mikutano ya Msigwa kutekeleza majukumu yake.
Kamati ya ulinzi na usalama inapofanya kazi za kisiasa. Nimesikia rafiki yangu DC Kasesera anautaka ubunge Iringa mjini. Namshauri kama anautaka atumie cheo chake cha uenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama vizuri. Sababu hajui vizuri watu wa Iringa. Mimi nilipata taabu sana kuwajua watu wa Iringa, baadaye nikawajua. Namshauri asome vizuri historia ya mkwawa. Wakiamua wameamua. Hawana maneno mengi ila wanavitendo. Utawajua wameamua kwenye matendo.
Vyombo vya dola vimepokea maagizo. Juzi Arusha Mkuu Majeshi alivitaka vyombo vya dola vijitoe kwenye siasa. Baadaye JPM akavitaka vijihusianishe kwenye siasa.
Siasa za upinzani kwa sasa ni ngumu sana hapa Tanzania. Lakini tumeamua kutonyamaza kimya. Lissu ametuongezea ujasiri. Hatuogopi lock up, hatuogopi magereza. Hatuogopi risasi. Bora kifo cha risasi kuliko kufa kwa ukimwi.
Namwambia Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi - Kasesera kuwa hatuogopi kesi za uchochezi. Tunafaida gani kustarehe wakati Lissu anapambania uhai wake. Mamia ya wanachadema wamefunguliwa kesi. Miili yetu ni kafara na dhabihu kwa Taifa na wana iringa.
CCM bila jeshi la polisi ni watamu kama uji wa mgonjwa. Msigwa endelea kuwanyoosha, usikate tamaa. Tuliamua wenyewe kuchagua fungu lililojema.

Maoni