MH LOWASSA AAPA BILA KATIBA MPYA AMNA UCHAGUZI MKUU 2020.

Wazir Mkuu Msaafu ameweza kukutana na mtanngazaji wa Voa Voive Of America Shaka ambaye alikuwa tanzania katika kongamano na mambo mbalimbali nchini pia ameweza kukutana na Mh Lowassa na kuweza kumsifu juu ya ukomavu wa kisiasa na kusimamia misingi ya bora kisiasa na kusema bila uvumilivu wake wa kisiasa nchi yetu kiamani ingeweza kuyumba,

Mh Lowassa ameweza kuongelea juu ya uchaguzi wa kenya na kuelezea kuwa ni uchaguzi wa kuigwa africa pamoja na dunia kwa kusimamia misingi ya kidomokrasia hasa africa ambapo nchi zake zimekuwa chini katika kusimamia misingi ya kidemokrasia tumejifunza mengi na tunatakiwa kujiweka sawa nasi tukawa mfano wa kuigwa,

Mh Lowassa ameweza kusema pia bila katiba mpya ndani ya nchi yetu basi 2020 amna mkuu maana ata tusipopiga kura watamtangaza raisi wao ambaye tume inamtaka na sio wananchi ambao wanapiga kura,

Tukipata katiba nzuri ya nchi na tume huru pamoja na kila mihimili ikajisimamia yenyewe bila kuongozwa namtu mmoja basi tunaweza kujenga taifa jipya la tanzania kama Bunge,vyombo vya dola na Mahakama wakatoa maamuzi yao na sio ya kiongozi flani,

Mh Lowassa amesema tukipata katiba mpya uchaguzi wa 2020 tutakuwa mzuri sana na tunatakiwa kujifunza kwa wenzetu wakenya wameweza kupiga maendeleo ni kutokana na katiba nzuri na sio kitu chengine kabisa kwahiyo tunatakiwa kujifunza kupitia majirani zetu ili nasi tuweze kupiga hatua kimaendeleo kama tuna kiu ya maendeleo kweli na sio kwenye midomo,

Kama chama cha chadema tunajipanga kuweza kusimama na watanzania wote na kutoa itikadi zetu za kisiasa ili kupata katiba ili iweze kusaidia taifa letu na kutuletea maendeleo zaidi katika siku za mbeleni,

Nawaomba wananchi wa Tanzania tusimame ili kuweza kupata katiba mpya ambayo inaweza kumsaidia mtanzania na kumsaidia kiongozi wa juu kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa pasipo kuwa na migongano na mtu yoyote.



Maoni