Mh Ummy Mwalimu, amempongeza Mstahiki Meya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

WAZEE WA UBUNGO WAFURAHIA NEEMA YA MATIBABU YA BURE KATIKA MANISPAA YA UBUNGO
Leo siku ya Jumatatu ya tarehe 04 september 2017, Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo, Mheshimiwa Boniface Jacob.
Amemkaribisha waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu, katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, kata ya Sinza Viwanja vya TIP.
Ambapo mheshimiwa Waziri, amezindua rasmi utoaji wa Kadi za Matibabu ya bure kwa wazee wote wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
Awamu ya kwanza wazee 7,299 wamenufaika katika kupata Vitambulisho hivyo, vitakavyo wasaidia wazee kupata huduma ya kumuona daktari,kupimwa na Matibabu ya dawa za aina zote watakazo hitaji.
Mtahiki meya amewashukuru watendaji wa Halmashauri, Wabunge na Madiwani wa manispaa ya Ubungo waliofanikisha kutenga bajeti ya billioni 1.8 ambayo itafidia huduma ya Matibabu ya bure kwa wazee wote wa Halmashauri ya manispaa ya Ubungo.
Aidha Mheshimiwa waziri, Ummy Mwalimu, amempongeza Mstahiki Meya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa kuwa Mfano wa kuigwa na kuingia kwenye orodha ya kipekee ya "MARAFIKI WA WAZEE" kwa kuwajali na kujitoa kwa ajili yao.
Mheshimiwa waziri ameahidi kusaidia Bima watoto 100, kama njia ya kuunga mkono juhudi za Halmashauri katika sekta ya Afya pamoja na kujenga Wodi ya mama na mtoto,chumba cha kujifungulia na vifaa vyake ndani ya mwaka huu 2017 kama njia ya kufurahishwa na kazi nzuri ya Halmashauri ya Ubungo.
MWISHO
Wazee wa Ubungo wamekubaliwa Ombi lao kwa Waziri kuwa vitambulisho hivyo watakavyopewa na Halmashauri ya Ubungo viweze kitumika katika hospitali za rufaa ikiwemo, Muhimbili na Jakaya kikwete ya Moyo kama njia ya muendelezo wa Huduma bure kwa wazee.
IMETOLEWA NA,
OFISI YA MSTAHIKI MEYA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO.




04 .09. 2017

Maoni