Mamia ya wakazi wa jiji la Los
Angeles, katika jimbo la Califronia wameruhusiwa kurejea makwao, baada
ya moto mkubwa wa nyikani ambao ulikuwa umeathiri eneo kubwa kuanza
kuthibitiwa.
Moto huo ulikuwa umeathiri eneo la ukubwa wa eka 5,000 na ulianza katika hori ya La Tuna Canyon siku ya Ijumaa.Kuzuka kwa moto huo kulisababisha kutangazwa kwa hali ya dharura.
"Tumepiga hatua kubwa, lakini bado haujadhibitiwa kabisa," Meya Eric Garcetti amesema, na akaonya kwamba hali huenda ikabadilika kutokana na kuwepo kwa upepo mkali
Betri mpya inayoweza kuzima moto
Afariki akichaji simu huku akioga kwenye bafu
Nyumba tatu ziliteketezwa na moto huo na inaarifiwa watu wanne wamejeruhiwa.
Moto huo ndio mkubwa zaidi kuwahi kuzuka katika historia katika eneo hilo.
Wakazi walikuwa wamehamishwa kutoka maeneo ya Glendale na Burbank lakini wakaruhusiwa kurejea baada ya mvua iliyokuwa ikinyesha bado na kuwepo kwa hewa baridi kuwasiadia wazima moto kuudhibiti.
Chanzo BBC
Maoni
Chapisha Maoni