NADHANI MAWAKILI WATAANZA KUELEWA MH LISSU ALIKUWA ANAMAANISHA NINI....

Siku chache zilizopita Rais wa TLS Mh Tundu Antipas Lissu aliwambia mawakili ni muhimu sana kushikamana kwenye tukio la Uvamizi wa Ofisi za Uwakili za IMMA lakini wengi hawakumuelewa wakahusisha kauli yake na mambo yao ya kisiasa. Leo tena Mh Tundu Lissu akiwa anapigania uhai wake Nairobi Hospital hapa nyumbani taarifa zinasema Ofisi zingine za Mawakili wanaomtetea Yusuph Manji zimevamiwa na watu wasiojulikana.
Tundu Lissu aliweza kusimamia juu ya kupigwa kwa Imma Advocates ila kuna baadhi ya watu walishindwa kumwelewa tumefika pabaya kwa namna ya matukio ambayo yanaendelea bila kukemea haya ni tatizo kubwa kwa taifa letu la tanzania, 
Nadhani kidogo kidogo mawakili wataanza kuelewa Tundu alikuwa anamanisha nini.
Watavamia katika ofisi za mawakili wakitoka huko wataenda kwenye ofisi za habari tusipokuwa makini na kuona ni kina nani ambao wanatenda haya,
Maoni ya wananchi wanasema kuwa wanaomba wawatambue hawa watu kabla ya wao kuchukua hatua ambazo wanategemea kufanya ,Masikitiko maeneo yote nchi juu ya matendo mbalimbali nchini.

Maoni