ONGEZEKO LA WANAFUNZI WENYE MIMBA LAKUWA NA WANAFUNZI WASEMA TATIZO KUBWA NI UCHUMI WA NCHI.

Uchumi wa nchi ndio umekuwa sababu kubwa za kupata ongezeko la wanafunzi wenye   mimba kutokana na hali za kifamilia kuwa duni siku baada ya siku kutokana na uchumi wa nchi kupolomoka wanafunzi wa ukerewe na baadhi ya mikoa wa mikoa wameweza kuweka sawa hili ni uchumi ukiendelea kushuka wanafunzi wengi wataweza kupata mimba kwani wanarubuniwa na watu wenye pesa na wakicheki maisha ambayo wanaishi inabidi wakubali,
Serikali ya Tanzania ipo wapi?

Hebu tutafakari kidogo, je, watoto wa kike kwanini hupata mimba nini hasa huwa kichocheo?
Kama nilivyosema hapo awali, wanafunzi hawa wakike huishi katika mazingira aidha yaliyo rafiki ama sio rafiki kwao. Hapa nitapenda kuangalia mambo kama umbali kufika shuleni, aina ya elimu inayotolewa shuleni, adhabu zitolewazo shuleni, mahitaji muhimu ya wanafunzi shuleni, umasikini, kukosa mlo wawapo shuleni, ukosefu wa vyumba vya kulala kwa wanafunzi watokao mbali, malezi hafifu, talaka, malezi kutokuwa ya jamii nzima, ombwe la maadili, elimu kutokuwa na mvuto, elimu isiyoleta matumaini ya ajira, tamaduni, siasa, ufisadi na mengine mengi.
Haya yote ni mazingira ama ya asili ama yale yakutengenezwa na mwanadamu yanaweza kuchangia yote kwa pamoja, ama kwa moja moja kwa asilimia nyingi sana mwanafunzi kupata mimba.
Tunapoamua kuwahukumu wanafunzi kwa kuwanyima fursa ya kusoma ni kanakwamba tunasema wanafunzi hawa wanaishi katika ulimwengu wao peke yao na hili ni kosa lao binafsi na sio kosa la mfumo wala mazingira.
Suluhisho la kweli katika vita dhidi ya mimba za wanafunzi ni kupambana na mazingira yanayowakumba wanafunzi wa kike badala ya kuendelea kuwakandamiza kwa kuwanyima haki ya kukosa elimu.
Endapo wanafunzi wa kike waliojifungua watakosa elimu ni dhahiri ya kuwa mzunguko wa umasikini utaendelea na kuongeza idadi kuwa ya watoto wa kike kutopata elimu na kuruhusu mgawanyiko baina ya wanawake na wanaume kuwa kubwa.
Nihitimishe kwa kusema, makatazo pekee sio suluhisho muhimu katika vita hii dhidi ya mimba za wanafunzi, bila kuyarekebisha mazingira yote yanayopelekea kuwepo kwa mimba za wanafunzi. Ni vyema sasa wizara ya elimu na idara zake husika itakafanya utafiti wa kina kugundua changamoto za kimazingira, binafsi na za kisaikolojia ili kuweza kuja na mbinu mbadala itakayokuwa na tija zaidi kwa watoto wa kike ili mapambano yawe ya kisayansi zaidi.
Bila Wasomi makini amna taifa imara.



Maoni