VIONGOZI wanne wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaomuunga mkono mwenyekiti wa chama hicho anayetambulika na Msajili wa Vyama, Prof. Ibrahim Lipumba wamefariki dunia usiku usiku wa kuamkia leo Jumatano September 6, 2017, baada ya msafara wao kupata ajali maeneo ya Ubenazomozi Mkoa wa Pwani.
Ajali hiyo mbaya imetokea wakati viongozi hao wakitokea Dodoma kwenye sherehe za kuapishwa kwa Wabunge wapya wa Chama hicho baada ya gari lao kugongana na Lori.
Taarifa ya Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdallah Kambaya viongozi waliofariki ni kutoka Wilaya ya Muheza, Tanga ambapo miongoni mwao ni Mgombea Udiwani wa Muheza Mjini, aliyefahmika kwa jina moja la Uredi.
Aidha, idadi ya majeruhi haijajulikana ila ni hawazidi 10 na baadhi yao wapo Hospital ya Tumbi huku akisema chanzo cha ajali hiyo ni gari la wafuasi hao kugongana na lori.
Tunamtafuta Lipumba aweze kuongelea zaidi juu ya ajali hii ambayo imeleta matatizo makubwa ila apatikani katika simu yake tutaendelea kumtafuta ili aweze kutoa maelezo zaidi juu ya hii Ambaye ni mwenyekiti ambayea alijiuzulu toka 2015 kuelekea kampeni za uchaguzi mkuu.
Maoni
Chapisha Maoni