TANZANIA:NGUVU KUBWA YA VYOMBO VYA DOLA KWA WAPINZANI YAENDELEA NA SASA KAKAMATWA MCH MSIGWA.

Kufuatia tukio la Mbunge wa Iringa Mjini na Mwenyekiti wa Chadema Kanda Ya Nyasa Mch Peter Msigwa kukamatwa na polisi jimboni iringa mjini alipokuwa anaongea na wananchi wa jimbo lake la iringa mjini kupitia mkutano wa hadhara jioni hii,
Katibu wa chadema kanda ya nyanda za juu kusini (Nyasa) Emmanuel Masonga ameonea kwa simu kuhusiana na sababu za kukamatwa kwa mbunge huyo na ameeleza kuwa wamemkamata mbunge kutokana na uchochezi alioufanya katika mkutano huo wa hadhara

Wakati huohuo Mstahiki Meya wa manispaa ya iringa mjini Mhe Alex Kimbe akiwa pamoja na mwenyekiti wa bavicha wilaya ya iringa Leonce Marto wakiwa pamoja na viongozi wengine wa chadema iringa pamoja na wananchi tayari wametafuta wakili ili ashughulikie suala hilo kufuatia wakili wa mbunge kuwa safarini nje ya mkoa,

Viongozi  hao walipoulizwa kinachoendelea wameeleza kuwa muda huu  mh mbunge msigwa anachukuliwa maelezo na polisi,

Maoni