UBINADAMU NDIO UMEWEZA KUMFANYA MH NYALANDU KUFANYA HAYA,,WATANZANIA WASEMA ANA ROHO NZURI SANA.

Mbunge Wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu (CCM).
Tunawaomba Wana Singida Na Watanzania Wote Tuendelee Kuchangia Gharama Za Matibabu Ya Mh. Tundu Lissu, Sote Tumkumbuke Katika Sala Na Dua Zetu Katika Majira Ya Saa Hii Ya Kujaribiwa Kwake. Mungu Akisema Ndio, Hakuna Anayeweza Kupinga. Kwa Wote Wanaohusika Moja Kwa Moja Kumtibu Na Kumtunza, Mikono Yao Na Fahamu Zao Zikahuishwe Katika Ubora Wote Wa Utabibu Na Matunzo.
Mazungumzo Yanayoendelea Na Madaktari Bingwa Na Hospitali Mahiri Kote Duniani Yafanikiwe Upesi Kumwezesha Mh. Lissu Kuifikia Huduma Bora Ya Matibabu Iliyopo Kwa Sasa Ulimwenguni.
Mh Nyalandu ameweza kutoa itikadi zake za chama na kuweza kuweka ubinadamu mbele ili kuweza kumsaidia Mh Lissu aweze kupona na kuendelea na mapambano katika nchi yetu mungu mkubwa atatenda na kuweza kumsimamia Ukiwa kiongozi alafu una ubinadamu mungu ataweza kukuongoza kwa kila jambo na kukuweza kukuvusha katika vipingamizi mbalimbali,

Maoni