WABUNGE WA UPINZANI NCHINI TANZANIA WAMESEMA BUNGE,MAHAKAMA NA VYOMBO VYA USALAMA AVIPO HURU NCHINI TANZANIA.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeweza kuendelea siku ya leo katika kikao cha Nane ya Bunge katika Makao makuu ya nchu na Ratiba ambayo iliyokuwepo siku ya mwanzo wa bunge leo siku ya jumanne ilikuwa ni 
Ratiba ya Leo Bungeni
 i/Kiapo cha Uaminifu
ii/Maswali
iii/Mswada ya Sheria ya Serikali     Kusomwa Mara ya Kwanza)
iv/Shughuli za Kamati

Wabunge wa upinzani waliweza kutoka baada ya ratiba za bunge kuanza kutokana na kutotambua uwepo na viapo vya wabunge wapi?wa cuf na kusema kuwa hao ni wabunge wa Lipumba na sio wabunge wa Cuf na kulaumu sana Mahakama,Bunge kushindwa kusimamia haki ambayo sasa wanashindwa na kumskiliza mtu mmoja anasemaje,

Wabunge wanasema bunge limeweza kuingiliwa na wabunge wanashindwa kusimamia haki na kubaki kuogopa sijui wabunge wa ccm wanashida gani/au ndio wanataka kuuwa upinzani maana hao wabunge sio halali kabisa na kusema kuwa ni genge la wahuni ambao wanapambana na upinzani wanchi hii chini ya Lipumba,

Wabunge wameweza kusema ingawa wamekula kiapo ila awataweza kuwatambua hao kama wabunge katika bunge la jamhuri na kusema mikakati ya kisheria inaendelea ili haki iweze kupatikana ,

Wameweza kusema kuwa watu wamejawa na hofu baada ya kusimamia kazi zao mbona jaji maranga wa Kenya aliweza kutoa hofu na kusimamia sheria leo hii anaandikwa katika historia duniani kwa kazi nzuri ambayo ameweza kufanya ila kwetu watu wanashindwa kujiamini katika kusimamia kitu na kubaki kupelekwa maana amekaa na uwoga,



Maoni