WANACCM WADAI KUWA CCM YA SASA IMEZIDI KUWA CHAFU AWAMU YA TANO NA CHADEMA KUZIDI KUWA SMART

CHADEMA INAVYONUFAIKA NA WATU SMART.
Na Thadei Ole Mushi.
#Hebu fikiria CCM inawezaje kufanya siasa na Chadema bila Dola? Hebu fikiria hakuna mamlaka yoyote ile kama polisi ambao wanaweza kustopisha mikutano, maandamano na plan zote za Chadema. Je CCM ya sasa hivi inaweza kupambana na CHADEMA kwenye uwanja wa Siasa? Jibu rahisi japokuwa kwa wengi hasa wana CCM wenzangu hawatanikubalia ni kwamba ni HAPANA.
# Kwa wiki kadhaa sasa pamoja na kwamba CCM tuna kila kitu pamoja na Dola ila CHADEMA wanatutoa kwenye reli na tunatumia muda mrefu sana kurudi. Tamko moja la Chadema tunaweza kushinda nalo wiki nzima kulidhibiti.......
#CCM WATU SMART WAMEPUNGUA.
#Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu Smart na Intelligent. Chadema wana watu Smart huku CCM wakijazana watu intelligent na wengine wabakia kuwa wapiga kura.
#Angalia sampling ya viongozi wa chadema ambao wanasumbuana na CCM ukiachana na Dr Mashinji hakuna mtu mwingine mwenye elimu inayofikia PhD wengi wana degree moja au mbili au hawana kabisa ila wapo very SMART.
Hapa nazungumzia wale ambao wanasmbuana ccm achana na kina Prof Safari na Baregu ambao wapo Passive sana.
Kuwa Smart ni kuwa na uwezo wa ku react kwenye situation yoyote ile na una react huku ukiwa sahihi kabisa yaani katika ku react kwako hukosei.
#Kuwa smart ni kuweza kupambana na Mazingira uliyonayo, ni ule uwezo wa kuwa tofauti na wenzako waliokuzunguka ni kuwa na uwezo wa kuweza kuona mbali kwa kutumia tu akili, ni kuwa na uwezo wa kutafsiri maneno au maandishi yaliyofichika nk.
#Angalia mara tu baada ya Mikutano ya hadhara ilivyokatazwa na kuruhusiwa ile ya kufanyia ndani ya Jimbo tu. Mara moja Chadema ilijibadili ikaanza mtindo wa matamko ambayo mengi yalisababisha viongozi wake kukamatwa na kufikishwa mahakani na kuachiliwa.
#Kwa kuwa kwa kipindi hiki wapo Smart wakatumia fursa hiyo ya kukamatwa kuitangazia Dunia kuwa nchini kwetu kuna Udikteta na viongozi wetu wanakamatwa kila siku. Nani huko njee atakayekuwa anabisha wakati kweli wanakamatwa? Iwe ni kweli wana makosa ama lah!! Ila kwao ile ilikuwa fursa.
#Angalia swala la Bombadia zetu na Swala la Makenikia walivyoreact baada ya kuona kuwa CCM itapata Credit kama watafanikiwa. Tulihangaika nao zaidi ya miezi kujibizana nao huku wakitumia weledi mkubwa sana wa kisheria kutudhibiti tukaishia kuwaita kuwa si Wazalendo baada ya hoja kutuelemea.
#Angalia hili la Uchaguzi wa Kenya walivyoitumia Fursa. Baada ya kuona kwa vyovyote Uhuru atashinda waliamua ku side naye mara moja. Waliside naye huku wakiwaaminisha kuwa Tanzania inawasaidia NASA. Tafsiri yake ni kuwa tumegombanishwa na wakenya bila kujua kwa vyovyote vile CCM haitaweza kuomba msaada Jubilee katika Chaguzi zake.... Chadema imewin hii situation nitakuja kuwaambia watanufaikaje na SYTEM YA Kenya.
#Kwa wanaoona Mbali utagundua hata Swala la mahakama ya Kenya kufutilia mbali Ushindi wa Kenyeta ni planned issue.... ili na huku tudai katiba kama ya Kenya na uhuru wa mahakama kama Kenya. Uhuru inawezekana alikaa na hawa watu wakakubaliana Mariga afute Uchaguzi kwa kuwa anajua atashinda tu ila Impact ya kufutwa kwake ni kuwaamsha watanzania kudai Katiba mpya... kwenye Siasa yote yanawezekana.
#Angalia wanavyolichukulia swala la Lisu kama Fursa. Ukiniambia Chadema wamekosa Fedha za Kumtibu Lisu nitakataa ni shilingi ngapi huwa wanapewa Ruzuku kwa mwezi? Ni kweli kuwa chama hakina Fedha?
#Angalia hii:- Chadema wameanza kuomba msaada wa matibabu kutoka Ujerumani, wakitoka ujerumani watenda marekani, baadaye wataenda Uingereza. Jambo hili litasababisha tuisipige hodi kwenye nchi hizi kabisa na linaweza kusababisha hata kuwekewa vikwazo.
#Hata hili la Kuhusishwa na Korea kaskazini ni kuanza kututafutia timing tu.... hii vita tuliyoianza tunapaswa kuwa makini....
#CCM inawezekana wamejazana maprofesa na watu wenye PhD ila wanabaki kuwa Intelligent tu na sio Smart. Kwa nini kila saa tunakamatwa kwenye kutoa ufafanuzi tu wa hoja za wapinzani? Lazma kuwa na watu wanaoweza kuwadrive Chadema na si wao watudrive.
#TRATEGY YA CHADEMA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
#Angalia Strategy yao katika kuchagua nani akagombee mahali... hawa kina Prof Jay na Sugu nani alijua walishawishiwa lini? Kwa sasa wameanza kumweka karibu Mwanamichezo Edo Kumwembe, huyu sio nyingi atakamata jimbo kwa tiketi ya Chadema dalili zote nimeshaziona labda aamue tu kubaki kwenye Sport. Akigombea huyu anapita moja kwa moja kutokana na kufahamika kwake.
#Roma Mkatoliki huyu yupo kwenye mipango ya Chadema kugombea soon mtasikia kashika jimbo haya yote yanapaswa kuonekana na watu smart ndani ya Chama na kutengeneza mipango ya kuzuia kugombea kwa ticket hizo.
#Baada ya Mzee Ndesamburo kufariki watu Smart ndani ya Chadema wameshajua kuwa nguvu ya chama itapungua kanda ya Kaskazini hivyo wameshaanza mipango ya kumtoa Mbowe kule Hai na kuna Plan za kugombea Jimbo la Moshi mjini.
#Chadema wanajua kuwa Nguvu yao kanda ya Kaskazini ipo kwenye majimbo ya Moshi mjini na Arusha mjini. Yaani ukishashinda haya hayo mengine yaliyobaki utashinda tu kwa kanda ya kaskazini kwa kuwa watu wa majimbo ya moshi mjini na arusha mjini ni Mobile kwa majimbo mengine yaliyobaki. Nikiwa na maana watu hawa wanaokuwa mjini mchana jioni wanakuwa kwenye majimbo ya vijijini. Kama Mbowe atasogea karibu na jimbo la Mwanga jimbo hili linaweza kupotea kabisa.
#Sioni wakiandaliwa watu wengine njee ya kina Chenge au tunasubiri wazee wetu Kina Chenge waendelee kuondolewa kama kina Wasira???
#Yapo mengi ya kuongelea eneo hili...
#JE CCM HAKUNA WATU SMART?
#Sijui na wala usiniulize... ila nitawapa mifano michache tu.
#Jimbo la Same Mashariki lilikuwa likiongozwa na Mama Ana Kilango. Ila ndani ya CCM huko huko same Mashariki alikuwepo mama mmoja anayeitwa NAGENJWA KABOYOKA huyu mama yupo very Smart aligombea kwa zaidi ya mara tatu kwenye kura za maoni CCM ila kwa Figusu na maelekezo ya Kamati kuu ya CCM Kilango alikuwa akimshinda.
Yule mama akachoka akaamua kujiunga CHADEMA na akagombea na kushinda kwenye Uchaguzi mkuu ni huyu ambaye ni Mwenyekiti wa PAC anayewasumbua pale Mlimani kwa hesabu Chafu.
#Wenzetu Chadema wapo vizuri sana kulinda watu wao Smart wadiondoke "Key players" hata kama hawana elimu kubwa sana ila wanajua kuwahifadhi.
#CCM ina tatizo eneo hili kuna watu wanajiona wanaweza kumbe hawawezi katika kiwango kinachohitajika. Kuna watu wapo njee ya Mfumo na wana mapenzi na CCM ambao wangeweza kutumika kuongeza nguvu kwenye chama na kupambana na hawa Chadema kwa akili kuliko Nguvu.
#Hizi Nguvu zitatutumbukiza kwenye shimo. Tukumbuke tu hakuna jambo lisilokuwa na Mwisho.
#Swali la kujiiza iweje chadema wanaongeza wabunge kila uchaguzi? Grafu ya kuongezeka wabunge inapanda kila kukicha bado kidogo itakuwa nusu kwa Nusu. Hiki ni kiashiria cha usmart wao.
#SINA MASLAHI NA NILICHOANDIKA.
Ole Mushi..

Maoni