WANANCHI TANZANIA WAELEZA SABABU YA DKT MAGUFULI KUZUIA MIKUTANO NA MAANDAMANO YA KISIASA NCHINI TANZANIA.
Raisi Magufuli ameweza kuzuia mikutano ya kisiasa na
maandamano kwa wapinzanii nchi nzima na wanasiasa kushindwa kujenga vyama vyao
na kuacha watanzania kuwa njia panda sana juu ya kufanya hivyo kwa Magufuli
kwani vyombo vya dola ndio vinasimamia kuzuia na kukamata kwa wote ambao
wanaokiuka agizo hilo na sio kukiuka katiba ya nchi,
Wananchi wa Tanzania wanasema kuwa sababu kubwa ya magufuli
kufanya hivyo ni baada ya uchaguzi mkuu 2015 kuona upinzani kuwa na nguvu kubwa
sana katika kampeni ambayo ilimfanya magufuli kufanya kampeni kwa shida sana
kila sehemu ya Tanzania kwa kupata upinzani mkubwa ,
Wananchi pia wanasema kuwa nguvu kubwa ambayo anayo #Lowassa
na upinzani kupanuka zaidi ndio sababu kubwa ambayo imeweza kumfanya Magufuli
kusimamisha mikutano ya kisiasa mpaka sasa,
Magufuli aliweza kutoa agizo kuwa ambao watafanya mikutano
ni wale ambao wameshinda ubunge au udiwani ndio watafanya mikutano tena katika
majimbo yao na kata zao na sio sehemu nyingine agizo hili lipo kinyume kabisa
na katiba ya nchi ila ni agizo la mtu,
Wananchi wanasema katika vyama vya siasa kuna viongozi wengi
ambao sio wabunge au madiwani kama chadema katibu mkuu Mashinji wa chadema sio
mbunge ila anatakiwa kukijenga chama ila leo mtu anatokea anasema amna siasa
mpaka 2020 wakati katibu mwenezi wa ccm Polelole anafanya mikutano sehemu mbalimbali mpaka
kwenye vyuo vikuu huu ubabe wan chi ya Tanzania kisiasa ni kutokana kutojiamini
kwa serikali ambayo ipo madarakani chini ya Magufuli
Wananchi wanasema
nguvu ya Lowassa bado ipo juu sana na umaarufu wa magufuli unazidi kushuka kwa
kasi kutokana na nguvu kubwa ambayo anachukua katika utawala wake.
Pia wananchi waliweza kusema kuwa wimbi la wanaccm kuondoka katika chama hicho kuamia upinzania kipindi cha kampeni akiwemo Mh Sumaye na Kingunge na wengi ambao waliweza kutoka ndio kitu ambacho kimeweza kufanya magufuli kuzaia mikatano na maandamano
Wananchi wa Tanzania wamesema rais wa nchi anavunja katiba ya nchi na kutoa maagizo yake binafsi.
Wananchi wa Tanzania wamesema rais wa nchi anavunja katiba ya nchi na kutoa maagizo yake binafsi.
Ni maoni ya wananchi mbalimbali ambao nimeweza kuwatembelea.
UWS MEDIA
Maoni
Chapisha Maoni