Kauli ya magufuli.
Nilipoingia madarakani sukari ilikuwa inauzwa Shilingi 5,000/= kwa kilo, lakini sasa hivi imeshuka na itaendelea kushuka zaidi." JPM, 23/09/2017, Arusha.
Wanaharakati wameweza kutoa ufafanuzi zaidi juu ya hutuba yake akiwa arusha Tarehe 23/9/2017
Wakati JPM anaingia madarakani mwaka 2015 sukari ilikuwa TZS 1,500/= hadi 1,600/=, kwa kilo moja. Maamuzi ya kukurupuka kuzuia sukari kutoka nje, wakati viwanda vya ndani havitoshelezi demand ya soko, yakafanya sukari ikapanda maradufu and still hatujarecover hadi sasa. Leo sukari ni TZS 2,500/= hadi 3,000/= kwa kilo. Sasa kwanini JPM anasema uongo hadharani?
Na kama anaweza kudanganya jambo la wazi namna hii, itakuaje kwa mambo mengine tusioyajua? Nimestaajabu sana. Aisee muogope sana mtu anayeongea uongo hadharani tena kwa kujiamini. Huyu ndiye anayejita mpenzi wa Mungu?
Wanaharakati wameweza kutoa maoni yao pia kuhusu kazi za serikali na kazi za chama
JPM usichanganye majukumu yako ya kisiasa na ya Kiserikali. Pesa za walipa kodi watanzania zinatumika vibaya.
Inakuwaje JPM anafanya siasa za chama chake katika Mikutano ya Kiserikali? Mikutano ya wananchi? Kwa kawaida ziara za Rais hugharamiwa na fedha za watanzania wote bila kuangalia kama ni mwanaCCM au chama kingine cha siasa.
Siasa ya namna hii ya JPM haikubaliki? Unapokeaje wanachama waliohama toka chama kingine katika mkutano wa kiserikali, mkutano wa wananchi?
JPM pia anajikaanga kwa kuwapigia debe madiwani hao waliohama toka CHADEMA kwa kuwaomba viongozi wa CCM wawape nafasi za kugombea kupitia chama cha CCM; Hii maana yake nini?
Hii maana yake ni kwamba tayari JPM anakiuka utaratibu na kanuni za uongozi na uchaguzi ndani ya chama chake kwa kutoa maelekezo yanayoashiria kuwatenga WanaCCM wengine kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi wa ndani wa chama hicho! Mwenyekiti wa Taifa wa chama anayehubiri maadili na CCM mpya leo anafanya haya kwa kutamka!
Yuko wapi HUMPHREY POLEPOLE anayeshadidia kuwa chini ya JPM kuna CCM mpya inatengenezwa ? Chini ya JPM hakuna CCM mpya bali CCM inayorudi kwenye mfumo wa " Zidumu fikra za Mwenyekiti" hii ndiyo CCM inayojengwa chini ya JPM na wanaCCM mnapaswa kulitambua hili.
Nikirejea kwenye matumizi isivyo sahihi za pesa Umma, JPM anapaswa kutenganisha ziara zake za kisiasa na Kiserikali. Anapaswa kuishi kwa kile anachokihubiri na isiwe ni usanii wa kudanganya umma kwamba tunapigania maslahi ya wanyonge ilhali wanyonge hao ni WanaCCM milioni 6 na si Watanzania milioni 54!
Kwenye Mkutano wa kuwa Commission Maafisa wa Jeshi na Mkutano wa wananchi kama ilivyokuwa agenda ya mkutano huo, Rais anafanya siasa, anapokea wanachama wapya ? Hii ndio Tanzania inayorudi miaka 50 nyuma katika demokrasia chini ya JPM!
Tunahitaji matumizi sahihi ya kodi zetu, ni lazima watanzania tupaaze sauti tuseme kwa vinywa vyetu na maneno makali: "Tunahitaji Matumizi sahihi ya fedha zinazotokana na kodi zetu"
Ghafla nimemkumbuka kaka yangu Tundu Lissu, najua angelisemea hili pia. Mungu amponye haraka arudi kuendelea na majukumu ya kutetea na kulinda rasilimali za nchi yetu.
Maoni
Chapisha Maoni