WATANZANIA WATAKA RASIMU YA WARIOBA BAADA YA KATIBA YA SASA KUSEMA NI MBOVU,RAISI APUNGUZIWE MADARAKA

KATIBA ya Tanzania ni mbovu. Hali hiyo imekuwa ikitumiwa na serikali kufanya uamuzi wenye msukumo wa kichama zaidi, anaandika Faki Sosi.
 
Kibata Peter, Wakili na Mwanaharakati wa Haki za Binaadamu Tanzania amesema kuwa, zuio la mikutano ya vyama vya siasa nchini lililotolewa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) linatokana na kutokuwa na Katiba nzuri.

Amesema kuwa, kutokana Katiba yetu, rais aliyepo madarakani ndiye anayeteuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) na makameshna wengine wa tume ambao hutokana na itikadi yake.

“Angalia mazingira haya, rais anayetokana na chama cha siasa ndiye anayeteua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.
“Hawezi kumteua mtu ambaye hawafanani itikadi, sasa katika mazingira haya unategemea nini wakati wa uchaguzi?” amehoji.


Maoni