Wadau wa Timu ya Njombe Mji jana waliweza kukutana katika
ukumbi wa Turbo Njombe mjini kuweza mikakati ya kuweza pointi tatu katika mechi ya kesho kutwa
jumatano katika uwanja wa sabasaba njombe mjini,
Kikao cha wadau wa Njombe Mji kiliweza kuongozwa na
mwenyekiti wa club ya Njombe Mji na wajumbe wa club pamoja na kamati ya ufundi
ili kuweza kujua jinsi gani?wataweza kuchukua pointi tatu,
Mwenyekiti wa club amesema timu ipo viziri kwasasa na
tusahau mechi ya kwanza zidi ya prison ambayo iliweza kufungwa 2 kwa 1 ila ni
kutokana na mikakati ilikuwa ijakamilika na wachezaji wao wengine walikuwa
wajakamilisha usajili wao pia ambao kuna wanigeria na mnyarwanda
Mwenyekiti ameweza kueleza timu ipo vizuri ila ijaweza
kupata mzamini wa kudumu kama wenzao singida united na club nyingine ingawa
tumetuma proposal sehemu mbalimbali mpaka sasa tujapata majibu kwahiyo
tunajibana hivyohivyo kutokana na hari yetu ambayo tunayo na
Mwenyekiti aliweza kusema tunatakiwa kujipanga katika
kushangilia timu yetu ingawa ninajua hapa kuna wanayanga wengi na wanasimba
kwahiyo uyanga tuweke pembeni na kuweza kuweka uzalendo wa timu yetu katika
kushangilia pasipo kukata tama,
Mwenyekiti ameweza kuwaimiza mashabiki wa mpira na wapenzi
wa njombe mji kuweza kufika mapema sana uwanjani ili kuweza kusaidia katika
kushangilia na kupanga mikakati ya ushangiliaji kwani tupo nyumbani tunatakiwa
kuonyesha tupo nyumbani ili kuweza kuwapoteza nguvu hawa wapinzani wetu,
Pia Wadau wa njombe mji waliweza kuchangia pesa juu ya Club
yao kuweza kufanikisha mipango mbalimbali ambayo ni faida kwa club yao kwenye
mambo mbalimbali ya Club
Wadau wa Njombe Mji pia waliweza kutoa maoni mbalimbali juu
ya kuboresha club yao iweze kukaa sawa na kuweza kufanya makubwa katika ligi
kuu ya Tanzania na kuchukua nafasi nzuri katika msimamo wa ligi hapo mbeleni
ingawa ndio mara ya kwanza kuingia maana miaka mingi imepita toka Nazareti
kutoka katika ligi kuu Tanzania
Maoni
Chapisha Maoni