Dunia mpya ya uongozi badala ya utawala ni dunia inayoshirikiwa na watu na sio mtu, Ulimwengu umefanya mageuzi makubwa katika nyanja za uongozi na kuongoza ambapo sasa umma unaamua juu ya hatima ya nchi au taasisi zao badala ya nyakati za ujima ambapo watawala walifikiri na kuamua kwaniaba ya umma, nauamuzi wao uliumiza umma.
Kuongoza ni kuonyesha njia kwa vitendo, kipimo cha uongozi ni jinsi gani kiongozi anaweza kuleta ushawishi kwa watu na kufikia maendeleo bora.Kiongozi bora hana muda wa kulalamika bali anatafuta ufumbuzi wa matatizo ya watu yaani wananchi wake. Kiongozi bora akiongea watu HUSIKILIZA, HUSHIKA NENO LAKE NA KULITENDEA NENO HILO.
Uongozi ni dhana,taaluma inayompa muhusika madaraka na uwezo wa kuwawezesha wale wanaongozwa kuunganisha nguvu,stadi na vipaji vyao na kuvitumia ili kufikia malengo yao. Kuongoza ni kujua lengo la wale wanaoongozwa na njia ya kufikia lengo lao. Kuongoza na kutawala, haya ni mambo mawili tofauti kabisa.
1. Kuna njia nyingi za kuainisha uongozi lakini njia ya msingi ni:
a). Kuangalia jinsi kiongozi alivyoingia madarakani na utaratibu wake wa kuongoza.
2). Kuna viongozi wapo Wafalme, Marais, Mawaziri, Watemi, Machifu, Wakurugenzi n.k. Viongozi wote hawa tunaweza kuwagawa katika mafungu yafuatayo:
1.1). Kutokana na jinsi walivyoingia madarakani na namna wanavyoongoza kama ifuatavyo:-
a). Wale wanaopata uongozi kwa kurithi.
b). Wanaopata uongozi kwa kuchaguliwa na watu
c). Wanaojitwalia mamlaka ya kuongoza kwa nguvu.
d). Wanaoteuliwa na mamlaka za juu zaidi.
b). Wanaopata uongozi kwa kuchaguliwa na watu
c). Wanaojitwalia mamlaka ya kuongoza kwa nguvu.
d). Wanaoteuliwa na mamlaka za juu zaidi.
Kiongozi anayeingia madarakani kwa moja wapo ya njia zilizotajwa juu anaweza kutumia mtindo wake wa uongozi.
Ipo mitindo miwili ya uongozi ambayo ni:
i). Uongozi wa kiimla (kidikteta).
ii). Uongozi wa kidemokrasia.
Uongozi wa kiimla ni mtindo wa kuongoza ambao kiongozi huongoza kwa amri bila kushirikisha watu wengine katika kufanya maamuzi. Mara nyingi uongozi wa aina hii haulengi katika kukidhi maslahi ya walio wengi, bali tu ya yule anayeongoza na wale wanaomlinda yaani wapambe wake.
Uongozi wa kidemokrasia ni ule wa kufuata katiba na sheria zilizowekwa na umma, kushirikisha watu katika kufanya maamuzi na utekelezaji wake. Kwa kawaida viongozi wa aina hii hulenga katika kukidhi mahitaji ya walengwa.
Kiongozi ni lazima aishi na kutembea katika sifa sahihi za kiongozi bora ambazo ni:
1). Kiongozi ni lazima awe na ufahamu mkubwa juu ya taasisi anayoiongoza, malengo yake, mazingira na matatizo yake.
2). Uaminifu na kila taasisi inalenga kufikia lengo fulani. Ni wajibu wa kiongozi kuwaongoza wana taasisi ili wafikie malengo yao. Kwa hiyo kiongozi ni lazima aweze kubuni mikakati na mbinu zitakazoiwezesha taasisi anayoongoza kufikia malengo yake.
3). Kiongozi ni lazima akubalike katika jamii na taasisi anayoiongoza. Ili akubalike ana budi kuzingatia maadili ya msingi ya jamii na taasisi yake. Kiongozi mnafiki, mwongo, mlevi, mvivu, asiye mwaminifu n.k hawezi kuwa kiongozi mzuri.
4). Kiongozi ni vema zaidi awe mcha Mungu japo sio lazima..
Hakuna serikali ya mtu duniani inayofanikiwa, bali serikali ya watu hufanikiwa...Linalojamba ni tumbo, makalio ni spika tu.
Kuna watu wasipokuelewa maneno na matendo yako, mshukuru Muumba wako, wewe bado unafikra chanya, wakianza kukuelewa jichunguze ni wapi umeanguka maana umeanza kuwaza kama wao.
Maoni
Chapisha Maoni