Zimbabwe nao walilia Demokrasia wapongeza mahakama ya Kenya

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai ameupongeza uamuzi wa Ijumaa wa mahakama ya juu nchini Kenya kwa kuamuru kufanyika kwa uchaguzi mpya kwa kusema ni hatua njema kuelekea demokrasia.
Tsvangirai ambae ni kiongozi wa chama cha MDC ameshindwa mara tatu katika jaribio lake la kuwania urais wa Zimbabwe na mara zote dhidi ya kiongozi wa muda mrefu Rais Robert Mugabe. Akizungumza katika mkutano na maelfu ya wafuasi wa muungano wa vyama vya siasa vya upinzani kuwa uamuzi uliochukuliwa na mahakama ya Kenya sio wa kawaida barani Afrika.

Mwaka 2008, Tsvangirai alimshinda Mugabe katika duru ya kwanza lakini hakufanikiwa kuibuka na wingi wa kura, na kusababisha uchaguzi huo urudiwe. Lakini baadae alijiondoa katika mchakato kutokana na kutokea vurugu dhidi ya wafuasi wake.

Maoni