Beki wa Barcelona Gerard Pique
amesema atastaafu soka ya kimataifa kabla ya Kombe la Dunia iwapo
ataendeleza kukosolewa kwa kuunga mkono kura ya maoni ya uhuru wa jimbo
la Catalonia.
Barcelona walilaza Las Palmas 3-0 katika mechi
iliyochezewa uwanja usio na mashabiki Jumapili baada ya maandamano
kukumba jiji la Barcelona.Mchezaji huyo wa miaka 30 alitaja mechi hiyo kuwa "ngumu zaidi" kwake.
Nafikiri ninaweza kuendelea," alisema Pique.
Lakini iwapo bodi inafikiri kwamba mimi ni tatizo, nitachukua hatua na kuondoka timu ya taifa kabla ya 2018."
"Kuna watu wengi sana Uhispania ambao hawakubaliani na yale yaliyotokea leo na wana imani katika demokrasia."
Catalonia, jimbo la watu takriban 7.5 milioni kaskazini mashariki mwa Uhispania, lina lugha na utamaduni wake.
Barcelona ndio mji mkuu wa jimbo hilo ambalo linajivunia uhuru kiasi lakini halijatambuliwa kama taifa huru chini ya katiba ya Uhispania.
Kuzomewa Uhispania
Pique
amechezea timu ya taifa ya Uhispania mara 91 lakini amezua utata
kutokana na msimamo wake kuhusu kura ya maoni ya kujitenga wka
Catalonia.Wakati wa mechi yao ya kirafiki dhidi ya Columbia mjini Murcia, mji ulio kusini mashariki mwa Uhispania, alizomewa na mashabiki wanaopinga uhuru wa Catalonia.
Beki wa Real Madrid Sergio Ramos ameingilia kati na kuwataka mashabiki wamheshimu mwenzake huyo katika timu ya taifa.
Kabla ya mechi hiyo ya Jumapili dhidi ya Las Palmas, Pique alipakia kwenye Twitter picha iliyomuonesha akipiga kura katika kura hiyo.
Maoni
Chapisha Maoni