Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA)Jimbo la Segerea wameendelea kuivunja ngome ya CCM




Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) lavunja ngome ya Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT)*
Jana tarehe 07/10/2017 Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA)Jimbo la Segerea wameendelea kuivunja ngome ya CCM Kata ya KIWALANI ambapo kupitia kikundi cha kusaidiana kilichoanzishwa na Uongozi wa BAWACHA Jimbo chini ya mwenyekiti Agnesta LAMBERT kimekuwa kivutio kwa wanawake wengi na hivyo wanawake hao wa CCM kuamua rasmi kujiunga na CDM, maana wameona huko ndiyo watetezi wa wanyonge walipo!
Baada ya tukio la kuchukua kadi kufanyika, wanawake hao waliomba wasajiliwe katika Msingi wao maana wote wanatoka eneo moja (Mtaa wa Yombo)
Mwenyekiti wao aliwaomba wavumilie mpaka kesho (leo) tarehe 08/10/2017 ili Uongozi wa BAWACHA Kata uwasiliane na Uongozi wa Chama Kata ili waje kuwasajili rasmi.
Leo tarehe 08/10/2017 jambo hili limefanikiwa ambapo Uongozi wa Chama Kata umefika pale wanawake wanakokutania kila jumapili ili kumaliza kiu yao.
Zoezi hili limefanyika chini ya mwenyekiti Agnesta LAMBERT (BAWACHA), Uongozi wa BAWACHA Kata ya Kiwalani na viongozi wa kata Chama (Mwenyekiti wa Kata, Mwenezi wa Kata, Mwenyekiti wa Mtaa huska pamoja na Katibu wake).
Uongozi wa BAWACHA Segerea kipekee sana wanawashukuru sana viongozi wa Chama Kata ya Kiwalani kwa mshikamano waliouonyesha. Mungu awabariki sana!
Wanawake waliosajiliwa ni zaidi ya 30! Kwa style hii mpaka tufike 2020 CCM watabaki watupu.
Mungu Ibariki CHADEMA! Mungu Ibariki BAWACHA!
Imetolewa na
Agnesta LAMBERT 
Mwenyekiti BAWACHA Segerea.

Maoni