Cristiano Ronaldo amkalisha tena Messi Tuzo za Fifa 2016/2017.



Kwa mara ya pili Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya The Best Fifa awards baada ya kupata 43% ya kura zilizopigwa huku akimuacha mbali mpinzani wake mkubwa Lioneil Messi aliyepata 19%.

Msimu uliopita Cristiano Ronaldo alifunga mabao 12 katika Champions League huku akifunga mara mbili katika mchezo wa fainali na kuwasaidia Real Madrid kutetea kombe la Champions League.
Manahodha waliompigia kura Cristiano Ronaldo ni pamoja na Luca Modric, Sergio Ramos, na Marcelo huku Neymar, Iniesta na Suarez wakimpigia kura Lioneil Messi. Wakati Ronaldo akitwaa Best Male awards kocha wake Zinedine Zidane aliwabwaga Massimiliano Allegri na Antonio Conte na kutwaa tuzo ya kocha bora wa FIFA.
 
Leo katika Jiji la London, habari kubwa inayohusu michezo ni utolewaji wa tuzo za wanamichezo bora wa mwaka wa shirikisho la soka duniani FIFA - The Best.
Pamoja na vipengele mbalimbali kuwepo ila macho na masikio ya walio wengi yapo kwenye tuzo ya mchezaji bora wa soka upande wa Wanaume! Walioingia fainali ni mshindi wa mwaka uliopita Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Neymar.
Nikiwa hapa jijini London nitakuletea kila linalojiri katika siku hii kubwa ya soka duniani.

Maoni