HAKUNA NYONGEZA YA MISHAHARA WALA AJIRA MPYA HADI TUHAKIKI UMRI NA WAZIRI MKUCHIKA.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kepteni George Mkuchika amesema serikali ina mpango wa kuongeza mshahara kwa watumishi wake na kuta-gaza ajira mpya lakini haitafanya hivyo hadi kwanza ihakiki umri wa watumishi waliopo kazini.
Mkuchika amesema watumishi elfu 40 wamebainika kugushi umri wa kuzaliwa.
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo Angella Kairuki, Mkuchika amesema kutokana na hali hiyo serikali haitapandisha mishahara hadi hapo zoezi la uhakiki litakapokamilika.

Kuna watu wameghushi umri wao wa kuzaliwa. Hawa lazima tuwatoe kwanza kabla hatujaajiri wengine na kuongeza mishahara. Alisema Mkuchika.
Mkuchika amedai kwamba kuna watumishi 40, 000 wamefoji umri kwa hiyo watafanya uhakiki kwanza na kuchukua hatua kabla ya kupandisha mishahara
Maoni
Chapisha Maoni