Mwadhama Kadinali, Polycarp Pengo amesema kwamba kauli iliyotolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo la Rulenge mkoani Kagera, Severine Niwemugizi kwamba Katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi ni maoni binafsi siyo msimamo wa Kanisa !
Mtu akiniambia priority ya Tanzania ni Katiba mpya inabidi anithibitishie huo ukipaumbele maana siwezi kuona mtoto anakufa kwa njaa au kwa kukosa dawa eti kwa sababu ya Katiba mpya. Kwangu mimi Katiba ni kitu ambacho kije baadaye, si cha haraka."
MAONI YA WANANCHI
Ni kweli sio tamko la Kanisa maana kanisa limekuwa bubu katika uovu mwingi nchini. Nakumbuka Kanisa lilivyotoa nyaraka nyingi kushinikiza Katiba Mpya wakati wa JK mpaka kuleta mvutano na watu wa Imani nyingine. Kanisa halijawahi kubatilisha. Labda alionewa Mrisho na sasa ni Joseph!
Halikadhalika hata aliyoyaongea Pengo nayo ni maoni yake binafsi pia maana nae sio msemaji wa Kanisa. Na bila shaka, hata ile kesi dhidi ya Gwajima ilikuwa ya Serikali na sio ya Pengo!
Ingepaswa aheshimu tu maoni ya mwingine kama anavyotaka na yake yaonekane ni ya Kanisa.
It Is Very Unfortunate Kadinali Hajui Kinachoendelea Nchini.. Hatari sana! Anyway, labda bado mgonjwa!
Maoni
Chapisha Maoni