Mmoja wa maafisa wakuu wa Tume ya
Uchaguzi Kenya (IEBC) Dkt. Roselyn Akombe ametangaza kujiuzulu katika
tume hiyo chini ya wiki moja kabla ya uchaguzi mpya wa urais kufanyika
nchini humo.
Dkt Akombe ametuma taarifa kutoka mjini New York
anakoishi ambapo alikuwa akiufanyia kazi Umoja wa Mataifa kabla ya
kujiunga na tume ya IEBC.Katika taarifa, Dkt Akombe alisema kuwa merejeleo ya uchaguzi utakaofanyika hayaafikii matarajio ya uchaguzi ulio huru na wa haki.
Uamuzi wangu wa kuondoka IEBC utawasikitisha baadhi yenu, lakini si kwa sababu nilikosa kujaribu. Nilijaribu kadiri ya uwezo wangu ukizingatia hali na mazingira yaliyopo. Wakati mwingine, unalazimika kusalimu amri na kuondoka, hasa wakati maisha ya watu yamo hatarini," amesema kwenye taarifa hiyo.
Tume sasa imekuwa kama sehemu ya mzozo wa sasa. Tume imo matatani.
Imekuwa vigumu kuendelea na mikutano ya tume ambapo Makamishna kila wakati wanalazimika kupiga kura kufanya maamuzi kwa kufuata msimamo wao badala ya kuangazia uzito wa jambo linalojadiliwa.
Maoni
Chapisha Maoni